Miongoni mwa ratiba ya (labbaika yaa Hussein), jumuiya ya Skaut ya Alkafeel ni moja ya idara za kiraia ya watoto na makuzi chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wanatoa huduma mbalimbali zikiwemo huduma za afya, katika ratiba yake ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), ambayo mamilioni ya watu wanamiminika katika mji mtukufu wa Karbala kwa ajili ya kufanya ziara hiyo.
Kuhusu swala hili tumeongea na kiongozi wa idara ya watoto na makuzi Ustadh Hasanaini Faruuq Alkhafaji, amesema kuwa: “Jumuiya ya Skaut Alkafeel inafanya kila iwezalo katika kuhudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake mbeba bendera wake Abulfadhil Abbasi (a.s), kama kawaida yake katika kila mwaka, kuna harakati nyingi za kielimu na kitamaduni pamoja na huduma mbalimbali zinazo tolewa kwa mazuwaru watukufu”.
Akaongeza kuwa: “Kutokana na changamoto ambayo dunia inapitia kwa sasa tunatekeleza maagizo yaliyotolewa na mamlaka husika, jumla ya wanaskaut (90) wamewekwa katika vituo vitatu, ambavyo ni: mji wa mazuwaru Alqami, uliopo kwenye barabara ya (Baabil – Karbala), chuo kikuu cha Al-Ameed chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye barabara ya (Najafu – Karbala), wamepewa jukumu la kupuliza dawa kwenye vituo hivyo na kugawa barakoa kwa mazuwaru, aidha kuna hema lenye vituo vingi tofauti, wanafanya kazi zaidi ya saa (12) kwa siku, muda wa kazi wameugawa katika vipindi viwili, asubuhi na jioni, na mwisho wa kazi hufanya majlisi ya kukumbuka matukio ya Ashura, na sababu za muhanga wa Imamu Hussein (a.s)”.
Akamaliza kwa kusema: “Sambamba na kazi zinazo faywa na jumuiya ya Skaut ndani ya miji tuliyo taja, kuna kundi la watu (60) wanaojitolea kufanya kazi na madaktari wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika maeneo ya karibu na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwenye milango yake mikuu, jukumu lao ni kuwapuliza dawa mazuwaru watukufu wanaokuja kwa baba wa watu huru Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya Arubaini, pamoja na kutoa huduma ya msaada wa matibabu ya dharura kama likitokea tatizo lolote la kiafya”.