Mafundi wa kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wamemaliza ujenzi wa daraja la chuma litakalo tumika kwa muda kupita mazuwaru wa Arubainiyya, wanaokuja katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, daraja hilo litarahisisha utembeaji wa mazuwaru na mawakibu za waombolezaji, na litaondoa msongamano baina yao.
Kiongozi wa kazi za ujenzi katika kitengo tajwa, Mhandisi Muhammad Mustwafa Twawiil ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tumejenga daraja kwa ajili ya kurahisisha upitaji wa mazuwaru na kuwafanya wasigongane na matembezi ya mawakibu za waombolezaji, pia daraja hili ni sehemu ya maandalizi rasmi ya ziara ya Arubainiyya ya Imamu Hussein (a.s), lipo upande wa kusini magharibi ya Ataba tukufu mkabala na mlango wa Imamu Hussein (a.s)”.
Akaongeza kuwa: “Daraja limetengenezwa kwa vyuma vilivyo unganishwa na kupandanishwa kwa njia maalum za kihandisi, vina upana wa (mita 8) na kuna sehemu mbili ya wanaokwenda na wanao rudi, kila sehemu inaupana wa (mita 4), urefu wake wa kwenda juu ni zaidi ya (mita 4), kunavipande vya mbao pia, kila kipande kinaurefu wa (mita 2.40) na upana wa (mita 1.22), vimewekwa pembezoni mwa daraja kwa ajili ya kulinda usalama wa mazuwaru wakati wa kupita kwao, daraja hilo ni msaada mkubwa kwa mazuwaru na mawakibu kwani linaondoa msongamano”.
Kumbuka kuwa kila mwaka kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu hujenga daraja, nalo ni moja ya madaraja matatu ambayo hujengwa na kitengo hicho, kuna madaraja mengine mawili hujengwa na kitengo cha ujenzi cha Atabatu Husseiniyya tukufu, kwa ajili ya kuondoa msongamano baina ya mazuwaru na mawakibu za uombolezaji.