Maagizo ya utaratibu wa kuimarisha ulinzi na utoaji wa huduma yametolewa na kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya na imehimizwa kuzingatiwa

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika nchi ya Iraq na ulimwengu wa kiislamu, kimetoa maelekezo ya ulinzi na utoaji wa huduma kwa mawakibu za uombolezaji na za kutoa huduma zitakazo shiriki katika ziara ya Arubaini mwaka huu (1442h), na kimehimiza uzingatiwaji wa maelekezo hayo, ambayo ni:

 • 1- Wahudumu wote wa mawakibu wanatakiwa kuswali kwa wakati, kila mmoja aswali sehemu alipo, haitakiwi kutumia vipaza sauti wakati wa swala, aidha katika mida mingine inatakiwa kudhibiti ukubwa wa sauti, na vipaza sauti vyote vizimwe saa sita usiku.
 • 2- Wahudumu wote wa mawakibu Husseiniyya wanatakiwa kuheshimu na kulinda utukufu wa Mkoa wa Karbala.
 • 3- Mawakibu zote zinatakiwa kuzingatia ratiba ya matembezi yao, kutokana na aina ya maukibu kama ni zanjiil au matam, mawakibu za zanjiil zitaingia katika siku mbili (16 – 17 Safar) na maukibu za matam zitaingia (18 – 19 Safar).
 • 4- Hairuhusiwi kuweka kambi ya maukibu kwenye eneo la bustani au katikati ya barabara, na inatakiwa kutunzwa miti inayo pendezesha mji wa Imamu Hussein (a.s).
 • 5- Maukibu zitaingia kupitia mlango wa Kibla katika malalo ya Imamu Hussein (a.s), hadi ndani ya haram, na zitatoka kupitia mlango wa Qaadhwi Hajaat unaotokea kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili kisha zitaingia katika Atabatu Abbasiyya halafu zitatoka na kurudi katika maeneo yao.
 • 6- Tunatoa taarifa kwa mawakibu zote kuwa hakuna ruhusa ya kusoma tenzi ndani ya haram zote mbili Husseiniyya na Abbasiyya ili kuepusha msongamano.
 • 7- Kiongozi wa maukibu anatakiwa aonyeshe kibali alichopewa na polisi wa mkoa wa Karbala pamoja na kitambulisho alicho pewa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
 • 8- Kiongozi wa maukibu ni muhusika mkuu wa kuhakikisha usalama wa watu wake, na anatakiwa kuzuwia kuingia kwenye maukibu yake watu asio wajua, na anatakiwa atangulize watu wanaojulikana wakati wa kuingia katika Ataba mbili walio tambulishwa kabla ya kuingia kwao.
 • 9- Vipaza sauti na kamera vitakaguliwa na watu wa ulinzi na usalama.
 • 10- Hairuhusiwi kubeba siraha za moto au vitu vyenye ncha kali au vifaa vya kunyunyiza maji.
 • 11- Hairuhusiwi kubeba picha ya kiongozi yeyote wa Dini au siasa ili kufanya ibada hii kuwa makhsusi kwa ajili ya Imamu Hussein (a.s).
 • 12- Hairuhusiwi kujikata (tatbiir) katika ziara ya Arubaini, kama hilo likitokea kiongozi wa maukibu atawajibishwa kwa mujibu wa sharia.
 • 13- Maigizo yasiyo endana na Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) hayaruhusiwi, watakao fanya hivyo watarudishwa waliko toka, kwa mujibu wa historia, msafara wa kurudi mateka na Imamu Sajjaad (a.s) haukushindikizwa na jeshi la Umawiyya wala hawakuwa wamefungwa na hawakupigwa.
 • 14- Hairuhusiwi kuinua fimbo na kupandisha bendera na mabango yasiyo endana na ziara ya Arubaini.
 • 15- Mawakibu zitapewa vitabu maalum katika vituo vya ukaguzi vya nje na ndani, ili kurahisisha uingizaji wa vifaa vyao vya maukibu, kupitia kiongozi wa uhusiano wa mawakibu za Husseiniyya vilivyo pitishwa na idara ya polisi ya mkoa wa Karbala.
 • 16- Kubaini sehemu inapoweka hema la maukibu iwe ndani au nje ya mji na kuchukua ahadi ya kulinda Ataba mbili tukufu pamoja na watu wanaokuja kufanya ziara.
 • 17- Kuheshimu maelekezo na ratiba ya kuingia maukibu iliyotolewa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kutoa ushirikiano kwa wahudumu wa Ataba mbili takatifu na watumishi wa mawakibu pamoja na askari.
 • 18- Hairuhusiwi maigizo ya kubeba vichwa au miili katika uombolezaji ndani ya vituo vya mawakibu, kwani kufanya hivyo kunadhalilisha na kupunguza heshima pia hakuendani na tukio.
 • 19- Mawakibu za kawaida zitaingia mwezi 15 na 16 Safar tu.
 • 20- Kila maukibu inatakiwa kuwa na kifaa cha zimamoto na ikiweke sehemu ya wazi kinapo wezo kutumiwa kwa haraka iwapo litatokea tatizo la moto Allah atuepushie.
 • 21- Kulinda barabara na mali za umma, ikiwa ni pamoja na njia za maji, pia haitakiwi kufunga hema katika njia za maji au kutupa taka sehemu hizo, na kutatiza njia ya maji kwa namna yeyote ile.
 • 22- Hairuhusiwi kupika kwa kutumia kuni, upishi wote utumie gesi.
 • 23- Hairuhusiwi kuchachanganyika na wanawake katika maukibu ya zanjiil na matam.
 • 24- Kila maukibu inatakiwa iweke bango la utambulisho juu ya mlango wake, bango hilo litakua na jina la maukibu pamoja na jina la kiongozi wao na namba zake za simu.
 • 25- Maukibu inaruhusiwa kuingia mara mbili, mara ya moja ya zanjiil na mara nyingine ya matam.
 • 26- Hali yeyote ya uvunjifu wa amani au tatizo la kiafya litakalo tokea karibu na maukibu, wenye maukibu hiyo wanawajibika kutoa taarifa kwenye kituo cha polisi au kituo cha afya kilicho karibu yao.
 • 27- Hairuhusiwi kubeba vitu vya kikabila na kupiga ngoma ndani ya Ataba mbili tukufu, pia hairuhusiwi kuingia na mikokoteni mikubwa inayo beba vipaza sauti, mkokoteni unatakiwa uwe na ukubwa wa (mt1 ubana kwa mt1.5 urefu).
 • 28- Wahudumu wa maukibu wanatakiwa kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa pamoja na soksi za mikononi.
 • 29- Inatakiwa kuwa na kibali cha afya ya mnyama atakaechinjwa katika maukibu kwa ajili ya kitoweo.
 • 30- Wahudumu wa mawakibu wanatakiwa kuondoa vifaa vyao vyote baada ya kumaliza msimu wa ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: