Kufungua mlango wa kushirikiana na Atabatu Askariyya katika kuendeleza sekta ya elimu

Maoni katika picha
Semina za kujenga uwezo zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu bado zinaendelea, kitengo cha maeneleo endelevu kimefanya semina ya kujenga uwezo, kwa walimu wa shule za Nuurul-Haadi ambazo zipo chini ya Atabatu Askariyya.

Kwa mujibu wa maelezo ya dokta Muhammad Hassan rais wa kitengo cha maendeleo endelevu kuhusu semina hiyo amesema: “Tunajitahidi kuifanya Atabatu Abbasiyya kuwa kinara wa kutoa huduma zote za kijamii kwenye miji tofauti, pamoja na kwenye sekta ya afya, malezi, na huduma mbalimbali, na leo tumeinua mkono wa kushirikiana na Atabatu Askariyya tukufu”.

Akaongeza kuwa: “Atabatu Abbasiyya imetuma ujumbe wa wakufunzi kutoka kitengo cha maendeleo endelevu na malezi na elimu ya juu, kwa ajili ya kwenda kutoa semina kwa watumishi wa kitengo cha malezi na elimu cha Atabatu Askariyya tukufu, ili kuwajengea uwezo walimu wa shule za Nuurul-Haadi (a.s) zilizo chini yake”.

Akafafanua kuwa: “Ugeni huo umeendesha semina kwa muda wa siku tatu, kuhusu njia za ufundishaji na uongozi wa shule, sambamba na mawasiliano ya intanet na namna ya kutumia program za kisasa katika ufundishaji kwa njia ya intanet”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: