Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimetoa ratiba ya mawakibu za (zanjiil) katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu husseiniyya katika nchi ya Iraq na ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimetoa ratiba rasmi ya mawakibu za uombolezaji (zanjiil) zitakazo shiriki katika Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) mwaka huu.

Rais wa kitengo hicho bwana Riyadh Ni’mah Salmaan amesema kuwa: “Viongozi wa mawakibu na vikundi vya Husseiniyya kutoka mikoa yote ya Iraq wanatakiwa kuheshimu muda uliopangwa kwenye ratiba, ukizingatia kuwa muda huo unaanzia kuondoka katika jukwaa (kituo) kilichopo karibu na maonyesho ya barabara ya Imamu Hussein (a.s), kisha kuingia katika Atabatu Husseiniyya halafu kwenda katika Atabatu Abbasiyya na kumaliza matembezi ya maukibu, tunatarajia kutokhalifu utaratibu huo tuliotaja kwa ajili ya kumtumikia Imamu Hussein (a.s) na mazuwaru wake watukufu”.

Akasisitiza kuwa: “Ni lazima kuheshimu maelekezo yaliyo tolewa na idara ya afya na yaliyo tolewa na kitengo hiki, kila maukibu inaruhusa ya kushiriki hadi mara mbili tu, moja ya (zanjiil) na nyingine ya (matam), kwa mujibu wa ratiba ya mkoa wake kama ilivyo tangazwa, kiongozi wa maukibu atagongewa muhuri unao onyesha mara alizo shiriki”.

Ifuatayo ni ratiba:

Safar 15 na 16 1442h.

Mawakibu za kawaida zitaingia kutoka mikoa yote.

16 Safar 1442h.

 • 1- Mkoa wa Naswiriyya na vitongoji vyake: Kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.
 • 2- Mkoa wa bagdad na vitongoji vyake: kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 5 asubuhi.
 • 3- Mkoa wa Najafu na vitongoji vyake: kuanzia saa 7 baada ya Adhuhuri hadi saa 8 mchana.
 • 4- Mkoa wa Diwaniyya na vitongoji vyake: kuanzia saa 2 mchana hadi saa 10 Alasiri.
 • 5- Kadhimiyya takatifu: kuanzia saa 10 Alasiri hadi saa 12 jioni.
 • 6- Mkoa wa Misaan: kuanzia saa 1 usiku hadi saa 3 usiku.
 • 7- Mkoa wa Diyala: kuanzia saa 3 usiku hadi saa 5 usiku.
 • 8- Nchi za kiarabu na kiislamu: kuanzia saa 5 usiku hadi saa 7 usiku.

17 Safar 1442h.

 • 1- Mkoa wa Basra na vitongoji vyake: kuanzia saa 1 asubuhi hadi saa 3 asubuhi.
 • 2- Mkoa wa Baabil na vitongoji vyake: kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 5 Adhuhuri.
 • 3- Mkoa wa Waasit na vitongoji vyake: kuanzia saa 7 Adhuhuri hadi saa 9 Alasiri.
 • 4- Mkoa wa Karkuuk na Nainawa na vitongoji vyake: kuanzia saa 9 Alasiri hadi saa 11 jioni.
 • 5- Mkoa wa Samawa na vitongoji vyake: kuanzia saa 1 usiku hadi saa 3 usiku.
 • 6- Mkoa wa Swalahu Dini na vitongoji vyake: kuanzia saa 3 usiku hadi saa 5 usiku.
 • 7- Nchi za kiarabu na kiislamu: kuanzia saa 6 usiku hadi saa 7 usiku.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: