Vituo vya Ashura: Yazidi asafirisha msafara wa mateka wa Imamu Hussein (a.s) kutoka Damaskas

Maoni katika picha
Wanahistoria wanasema kuwa Yazidi alifurahishwa na kuuwawa kwa Imamu Hussein (a.s) na wafuasi wake pamoja na utekwaji wa familia ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), na alionyesha furaha kwenye kikao chake, hakujali ukatili na vitendo vya ukafiri alivyo fanya, hadi akafikia hatua ya kukanusha wahyi wa Mtume Muhammad (a.s.w.w), baada ya wakosoaji wake kuwa wengi na kutambua kuwa njama yake imefeli, kwa kufanya mambo ambayo hata asiyekua muislamu hawezi kuyafanya, na akatambua yaliyotokea ni sehemu ya usia wa Muawiya kwake, pale alipo muambia: Hakika watu wa Iraq hawatamuacha Hussein hadi wamtoe, atakapo toka mmalize, hakika yeye ni mpole na anahaki kubwa.

Kitendo hicho cha ukatili kikakataliwa vikali na watu wa nyumbani kwake na wake zake, kila mtu akawa anamlaumu hadi wasiokua waislamu, hasa baada ya kuamrisha kuuwawa kwa balozi wa mfalme wa Roma na akasikia kichwa kikisema (Laahaula walaa quwata illaa billahi), katika riwaya inasemekana baada ya kufanya mauwaji hayo ya kinyama alisikia sauti katika anga ya Damaskas, hakupata sehemu ya kujificha ispokua alichoona ni kumlaumu ibun Ziyadi na kukaa mbaili na mateka wale.

Kwani aliogopa kupinduliwa, akamuambia Nuúmanu bun Bashiri swahaba wa Mtume (s.a.w.w): waandae hawa wanawake (mateka) na uwape mtu muaminifu na mwema pamoja na farasi na wasaidizi.

Imamu Swadiq (a.s) anasema: Aliondoka Imamu Ali bun Hussein (a.s) Sham akiwa na watu wa nyumbani kwake pamoja na kundi la watumishi alio watoa Yazidi waende pamoja na watu wa nyumba ya Mtume (a.s) wakiongozwa na Nuúmanu bun Bashiri Al-Answaari, wakiwa na kichwa cha Imamu Hussein (a.s) pamoja na vichwa vya wafuasi wake na wakavirudisha kwenye miili yao, Sajaad (a.s) alipofika Iraq akamuambia muongozaji wa njia tupeleke Karbala. Walipofika Karbala wakarudisha kila kichwa kwenye muili wake, na wakamkuta Jaabir kwenye kaburi la Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: