Zaidi ya maukibu 500 kutoka Iraq: Idara ya ustawi wa jamii imeanza kutekeleza ratiba ya ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imeanza kutekeleza ratiba ya ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ya mwaka huu 1442h.

Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Qassim Rahimu Alma’muri amesema kuwa: “Ratiba hii ipo chini ya utekelezaji wa makamo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Ustadh Maitham Zaidi, ameandaa mazingira mazuri ya kiidara, yanayo wezesha kupokea idadi kubwa ya mazuwaru ndani ya mkoa mtukufu wa Karbala”.

Akaongeza kuwa: “Mawakibu zinashindana kuhudumia mazuwaru wa Arubaini wanaokwenda Karbala katika mikoa yote ya Iraq, zinatoa huduma mbalimbali kulingana na uwezo wa kila maukibu”.

Akabainisha kuwa: “Ofisi za idara ya ustawi wa jamii za mikoani zimetuma maukibu za kutoa huduma katika mji mtukufu wa Karbala na kwenye barabara zinazo kwenda Karbala, zinatoa huduma ya chakula, vinywaji na kuandaa sehemu za kupumzika mazuwaru, kuna maukibu Zaidi ya (150) katika mji wa Karbala, huku zingine zaidi ya (350) zikitoa huduma kwenye mikoa mingine hapa nchini”.

Tambua kuwa mawakibu ambazo zipo chini ya idara ya ustawi wa jamii, mwaka huu zinatoa huduma kubwa inayo endana na mazingira ya janga la Korona, zimegawa kiwango kikubwa cha vifaa vya kujikinga na maambukizi, ikiwa ni pamoja na barakoa na vitakasa mikono, wamekua wakiwaba bure mazuwaru katika barabara zinazo elekea Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: