Maukibu (2982) zimeshiriki kuhudumia mazuwaru wa Arubaini katika mkoa wa Waasit

Maoni katika picha
Kiteno cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kimetangaza kuwa zaidi ya maukibu (2982) zimeshiriki kuwahudumia mazuwaru wa Arubaini katika mkoa wa Waasit, miongoni mwa hizo maukibu (355) zitashiriki kutoa huduma katika mkoa wa Karbala.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo hicho bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan aliyotoa kwenye mtandao wa Alkafeel, alisema: “Hakika maukibu hizo zilianza kutoa huduma kwa zaairu wa kwanza kuingia katika mkoa huu, ambao ni moja ya vituo vya mazuwaru wanaotoka mikoa ya kusini, maukibu zimeenea kwenye barabara zote zinazo tumiwa na mazuwaru, kuanzia kwenye mpaka wake na mkoa wa Misaan hadi kwenye mpaka na mkoa wa Diwaniyya na mwisho kwenye mpaka na mkoa wa Baabil, idadi tuliyotaji na maukibu zilizo sajiliwa rasmi na mamlaka husika ya mkoa, kuna makumi ya mawakibu ambazo hazikusajiliwa pamoja na nyumba za watu na huseiniyya zilizo fungua milango kupokea mazuwaru na kuwahudumia”.

Akasema: “Kuna maukibu (355) zimeenda Karbala kuwahudumia mazuwaru watukufu katika barabata zinazo elekea kwenye malalo mbili takatifu kupitia huseiniyya au kwa kujenga mabanda maalum ya kutolea huduma”.

Wahudumu wa maukibu hizi hufanya kazi usiku na mchana bila kuchoka, kwa lengo la kutoa huduma bora, huku wakitumia uwezo wao wote wa hali na mali katika kufanikisha hilo, maukibu hizo pia zinatoa ushirikiano mkubwa kwa sekta ya ulinzi na afya, chini ya mfumo maalum unaosimamia matembezi ya mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: