Matembezi ya milele yanaendelea kuelekea kibla ya wapenzi.. ripoti ya matembezi ya Arubaini kwa njia ya picha.

Maoni katika picha
Kila Arubaini Karbala hujaa huzuni, utukufu na ukarimu.

Arubaini sisi wapenzi wako na mazuwaru wako ewe bwana wangu.

Imamu Hussein (a.s) alisimama akiwa peke yake katika ardhi ya Karbala, akaita kwa sauti: (Hivi kuna wa kuninusuru aninusuru) sauti hiyo imebaki vizazi na vizazi, inatafuta mtu wa kuitikia, haitulii hadi iupate moyo uliojaa mapenzi ya Ahlulbait (a.s), nyoyo za answari wa wafuasi wao na wapenzi wao.

Wanusuru wa Hussein (a.s) wameitikia wito wake tangu walipokua katika migongo ya baba zao na matumbo ya mama zao, wameitikia kwa sauti moja: Labbaika.. wito wa Allah, japokua muili wangu haukukujibu ulipohitaji msaada, na ulimi wangu haukuitikia ulipoita, ulikujibu moyo wangu na masikio yangu na macho yangu, hivyo ndio walivyo answari wa Hussein (a.s) wanahuisha kumbukumbu yake, na wamepandisha bendera juu ya kaburi lake, haifutiki athari yake wala picha yake usiku na mchana, pamoja na jitihada za viongozi wa ukafiri na wafuasi wa upotevu kufuta, ndio athari yake inaongezeka zaidi.

Matembezi ya Arubaini yanaonyesha wazi mapenzi ya kweli, matembezi ya milionea yamejaza weusi katika barabara za Iraq huku zikipepea juu bendera za huzuni na uaminifu.

Kamera ya Alkafeel inakuletea picha za matembezi ya leo katika mkoa wa Diwaniyya, nazo ni sehemu ndogo sana ya makundi ya watu kutoka sehemu mbalimbali wanaokuja kumpa pole bibi Zainabu (a.s) na kumuahidi Imamu wao Abu Abdillahi Hussein (a.s), kufuata njia yake –njia ya watu huru- aliyo iandika kwa damu yake na damu ya watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: