Mgahawa wa nje wa Atabatu Abbasiyya tukufu unaendelea kuhudumia mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia wafanya kazi wake wote wa vitengo tofauti wanajitahidi kutoa huduma bora kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Arubainiyya, mazuwaru ambao wamesha ingia Karbala au wale ambao wako njiani kuelekea Karbala kwa kutumia barabara tofauti, ikiwemo barabara ya (Najafu – Karbala) ambayo kuna mgahawa (Mudhifu) wa nje wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Tumeongea na mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya bwana Jawadi Hasanawi kuhusu huduma zinazo tolewa na mgahawa huo, amesema kuwa: “Miongoni mwa maandalizi ya Atabatu Abbasiyya katika ziara ya Arubaini ni kuandaa vituo vya kutoa huduma tofauti, chakula, afya na maelekezo, katika pande kuu tatu (Najafu – Karbala/ Bagdad – Karbala/ Baabil – Karbala)”.

Akaongeza kuwa: “Barabara ya Najafu inaongoza kwa kuwa na mazuwaru wengi wanao kwenda Karbala, kwa hiyo inavituo vitatu vikubwa vya kutoa huduma, ukiwemo mgahawa (Mudhifu) wa nje wa Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaendelea kusema: “Mgahawa huo una sehemu mbili, sehemu ya wanaume na wanawake, unatoa huduma muda wote, watumishi wa vitengo tofauti wanashirikiana kutoa huduma kwenye mgahawa huo, kuna huduma ya kupumzika, chakula, vinywaji pamoja na maelekezo ya kiafya”.

Akafafanua kuwa: “Kutokana na kuwepo kwa tatizo la Korona mwaka huu wahudumu wa mgahawa huu wanachukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi wao na mazuwaru watukufu”.

Kumbuka kuwa mgahawa wa nje wa Atabatu Abbasiyya tukufu, huwahudumia mazuwaru wa Arubaini kila mwaka, nao ni kielelezo kikubwa cha ukarimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: