Watumishi wa idara ya usafi wanafanya kazi kubwa kudumisha usafi katika eneo lote la Atabatu Abbasuyya tukufu katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Watumishi wa idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya, wanafanya kazi kubwa ya kudumisha usafi katika eneo lote la Atabatu Abbasiyya wakati huu wa ziara ya Arubainiyya, wanafanya kazi muda wote.

Kiongozi wa idara hiyo Muhammad Ahmadi Jawadi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Watumishi wa kitengo chetu kama kawaida yao katika ziara kubwa ikiwemo hii ya Arubainiyya hufanya kazi kubwa ya kudumisha usafi kwa kushirikiana na watu wa kujitolea kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Watumishi wa idara hiyo muda wote wapo katika vituo vyao vya kazi, ambapo ni kwenye barabara zinazo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na zile zinazo elekea katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, sambamba na sehemu ya uwanja huo, kazi yetu ni kudumisha usafi katika maeneo hayo kwa kuondo uchafu muda wote”.

Akaendelea kusema: “Watumishi wetu wanaingia kazini kupitia zamu tatu, asubuhi, mchana na usiku, huku watu wanaojitolea tumewapanga katika zamu mbili, zamu ya kwanza kuanzia saa moja asubuhi hadi saa moja jioni na ya pili kuanzia saa moja jioni hadi saa moja asubuhi, ili kuhakikisha kazi inaendelea kwa muda wa saa 24”.

Akafafanua kuwa: “Mwaka huu tunatumia mbinu mpya katika kufanya usafi, tumeweka matenki ya taka katika sehemu tatu, na tukapanga watu maalum wa kuokota uchafu na kuutupa kwenye tengi katika kila sehemu, kwa lengo la kuhakikisha matengi hayo hayatatizi mazuwaru wakati wa kufanya usafi, jambo ambalo linaweza kuleta usumbufu katika harakati zao na kuhatarisha usalama wa matembezi yao”.

Akasema kuwa: “Watumishi wetu na watu wanaojitolea wanachukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi, sambamba na uzowefu mkubwa walio nao katika kuamiliana na mazuwaru kwenye ziara kubwa kama hii, tunafanya kazi kwa baraka za Mwenyezi Mungu mtukufu na Abulfadhil Abbasi (a.s), tunatekeleza ratiba yetu ya kuhudumia mazuwaru kwa umakini mkubwa”.

Kumbuka kuwa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa vitengo ambavyo vinamhudumia zaairu moja kwa moja, hufanya kazi kwa nguvu zote ili kuhakikisha wanatoa huduma bora zaidi kwa mazuwaru katika ziara mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: