Mawakibu za matam zimeanza maombolezo ya Arubainiyya ya Imamu Hussein (a.s).

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo Jumatatu (18 Safar 1442h) sawa na tarehe (6 Oktoba 2020m), zimeanza kumiminika mawakibu za matam kuhuisha kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) baada ya kumaliza mawakibu za zanjiil maombolezo yao, chini ya ratiba iliyopangwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Maombolezo hayo yanafanywa chini ya utekelezaji mkali wa kanuni za afya katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, unaofanywa na watumishi wa Ataba hizo, kama sehemu ya kuheshimu usia wa Marjaa Dini mkuu na maelekezo ya idara ya afya kuhusu namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan amesema kuwa: “Mawakibu za matam ni sehemu ya muendelezo wa uombolezaji wa mawakibu za zanjiil, ambazo hushiriki katika kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), ni makundi ya watu ambao katikati yao hukaa muimbaji wa kaswida za Husseiniyya, huimba kaswida za kuomboleza zinazo onyesha huzuni waliyonayo wapenzi wa Ahlulbait (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Hakika mawakibu za kuomboleza zimezowea kufanya hivyo kila mwaka, zimetengwa siku mbili za mawakibu za zanjiil na siku mbili za mawakibu za matam, huanza kumiminika katika Ataba mbili mapema asubuhi na huendelea hadi baada ya Magharibi na Isha, hushiriki maukibu kutoka mikoa tofauti ya Iraq, kila mwaka kitengo cha maambimisho na mawakibu Husseiniyya huandaa ratiba ya kuingia na kutoka kwa maukibu hizo”.

Kumbuka kuwa sehemu ya kuanza matembezi ya maukibu hizo ni katika barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s) hadi kwenye haram yake takatifu, huku wakiimba kaswida za huzuni na kuomboleza, kisha huelekea katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kupitia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: