Uchapishaji wa maelfu ya vipande vya utambulisho na kuvigawa kwa watoto na wazee

Maoni katika picha
Kitengo cha hazina katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimechapisha maelfu ya vipande vya utambulisho wa watoto na wazee katika ziara ya Arubaini, kwa ajili ya kuwalinda na kurahisisha upatikanaji wao pindi wanapo potea au kutoweka.

Rais wa kitengo cha hazina Ustadh Adnani Badayuwi amesema kuwa: “Kitengo chetu kina harakati tofauti katika ziara ya Arubaini, kinamajukumu mengi yanayo changia katika utowaji wa huduma nzuri kwa mazuwaru, miongoni mwa mambo tunayo fanya ni mradi huu ambao umekubalika kwa kiwango kikubwa, tumechapicha vipande vya utambulicho na kuvigawa kwa watoto na wazee kupitia vituo vilivyopo kila upande wa mji (Najafu, Baabil, Bagdad)”.

Akaongeza kuwa: “Vipande hivyo vya utambulisho vimetengenezwa kwa plastiki nyepesi, kuna sehemu ya kuandika jina la aliye kivaa, namba ya simu ya ndugu yake, sawa awe mtoto au mzee, au mtu mwenye mahitaji maalum, au mtu yeyote atakae hitaji, na anakivyaa mkononi kwake, utambulisho huo utasaidia kumtambua na kumsaidia atakapo toweka au kupotea”.

Akasisitiza kuwa: “Mbinu hii imesaidia kurudisha watoto wengi waliokua wamepotea kwa wazazi wao”.

Akamaliza kwa kusema: “Vipande hivyo vimewekwa pia katika vituo vya kusaidia waliopotea na walio potelewa vilivyo chini ya Atabatu Abbasiyya, watumishi wa kitengo chetu na wahudumu wa kujitolea ndio wanao simamia ugawaji wa vipande hivyo, tayali tumesha kabidhi watu wengi waliopotea kwenye vituo vya kusaidia waliopotea au kupotelewa, vilivyopo kwenye barabara zinazo elekea Karbala na barabara za ndani ya mji”.

Mazuwaru wengi wamepongeza utaratibu huu na kushukuru aliyebuni jambo hili na kulifanya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: