Kwa kuhudhuria kiongozi mkuu wa kisheria: Atabatu Abbasiyya tukufu imefanya majlisi ya kuomboleza matembezi ya mateka wa Imamu Hussein (a.s).

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya asubuhi ya Jumatatu mwezi (18 Safar 1442h) sawa na tarehe (6 Agosti 2020m), imefanya majlisi ya kuomboleza kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) ndani ya ukumbi wa utawala katika haram tukufu, ni desturi ya Ataba kila mwaka kufanya majlisi ya kuomboleza tukio hilo.

Majlisi hiyo imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na baadhi ya wahudumu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), wakiwa wametekeleza masharti yote ya kujikinga na maambukizi ikiwa ni pamoja na umbali kati ya mtu na mtu.

Majlisi ilifunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo fuatiwa na muhadhara uliotolewa na Shekh Abdullahi Dujaili, aliye zungumzia dhulma walizo fanyiwa mateka wa Imamu Hussein (a.s) baada ya tukio la Twafu, na namna ambayo utawala wa Umawiyya ulivyo wafanyia, aidha amezungumzia nafasi kubwa ya bibi wa subira Zainabu Kubra na Imamu Sajjaad (a.s), kwa namna walivyo utambulisha muhanga wa Imamu Hussein ulimwenguni.

Majlisi ikahitimishwa kwa tenzi za huzuni na majonzi kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s), katika kumbukumbu ya Arubaini ya bwana wa mashahidi (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: