Atabatu Abbasiyya tukufu imeongeza nidhamu na utaratibu wa kujikinga na maambukizi

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeongeza nidhamu na utaratibu wa kujikinga na maambukizi, kutokana na kukaribia kilele za ziara na kuongezeka idadi ya mazuwaru, kwa namna ambayo wanahakikisha kuwe na mjongeo mzuri usiokua na msongamano, nidhamu hiyo pia imetumika kuwalinda mazuwaru wa mawakibu za waombolezaji na kuhakikisha usalama wao.

Miongoni mwa mambo yaliyo imarishwa na kufanyiwa kazi ni:

 • - Kuteua milango maalum inayo tumika kuingia na kutoka mazuwaru wa kike tofauti na milango wanayo tumia mazuwaru wa kiume.
 • - Kuainisha sehemu wanazo takiwa kupita mawakibu za kuomboleza wakati wa kuingia na kutoka katika Ataba kwa namna ambayo hawatatizi harakati za mazuwaru.
 • - Kuweka watu wanao ongoza matembezi ya mazuwaru kwenye milango ya Atabatu Abbasiyya tukufu wakati wa kuingia na kutoka.
 • - Kutenga sehemu ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kufanya ziara wanaume peke yake, pamoja na kutenga sehemu za sardabu ya Imamu Hussein na Aljawaad (a.s) kwa ajili ya kufanya ziara wanawake pekeyake, sardabu hizo zina dirisha linalo gusana na ukuta wa haram takatifu.
 • - Kuweka idadi kubwa ya waongozaji ndani na nje wa haram tukufu kwa lengo la kuwaelekeza mazuwaru sehemu wanayo kwenda na kuhakikisha hawasimami njiani.
 • - Kuweka watu wanao ongoza matembezi ndani na nje ya haram wenye jukumu la kuhakikisha misafara ya kuingia na kutoka haisimami.
 • - Kuweka njia maalum ya kuingia na kutoka mawakibu za waombolezaji bila kutatiza harakati za mazuwaru.
 • - Kuongeza sehemu za kukagulia mazuwaru katika milango ya haram tukufu.
 • - Kuongeza kazi ya kuwapuliza dawa mazuwaru na mawakibu muda wote.
 • - Kuongoza idadi ya watoa huduma ya kwanza ya matibabu iwapo tatizo lolote la kiafya likitokea.
 • - Kuhakikisha matembezi ya nje ya haram yanaendelea vizuri kupitia waelekezaji wa misafara ya kuingia na kutoka, kwa ajili ya kurahisisha matembezi ya mawakibu.

Kumbuka kuwa watumishi wa malalo tukufu wanashirikiana katika kufanya kazi hii, kuna watumishi wa kitengo cha usimamizi wa haram, kulinda nidham, utumishi, idara ya masayyid na idadi kubwa ya watu wanao jitolea, kazi hii inaweza kuongezeka katika saa zijazo, ili kuhakikisha hautokei msongamano wa mazuwaru japokua idadi yao imeanza kuongezeka katika siku hizi, na kila tunapo karibia kilele cha ziara watu wanaongezeka zaidi, na kilele cha ziara hii ni usiku wa mwezi ishirini Safar na mchana wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: