Maukibu Ummul-Banina katika chuo kikuu cha Al-Ameed inatoa huduma tofauti kwa mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Maukibu ya Ummul-Banina (a.s) katika chuo kikuu cha Al-Ameed inatoa huduma tofauti kwa mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Arubainiyya, hususan wanaotumia barabara ya (Najafu – Karbala), maukibu hiyo inatoa huduma za maelekezo na elimu pamoja na sehemu ya kupumzika, chakula, vinywaji na zinginezo.

Bwana Maajid Rabii kiongozi wa maukibu ya Ummul-Banina ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Maukibu inasehemu mbili: ya wanawake na ya wanaume, kila sehemu inatoa huduma ya mapumziko na chakula sambamba na huduma za afya na matibabu, ikiwa ni pamoja na kugawa barakoa na kutoa maelekezo ya kujikinga na maambukizi, bila kusahau huduma ya tablighi na huduma za kielimu na kimalezi”.

Akaongeza kuwa: “Vitengo tofauti vya Atabatu Abbasiyya tukufu vinashiriki katika kutoa huduma hizo, kama vile kitengo cha dini, kitengo cha elimu na utamaduni, kitengo cha hazina na kitengo cha mgahawa (mudhifu)”.

Akasema kuwa: “Sisi tunaheshimu maelekezo yote ya kujikinga na maambukizi wakati wa kutoa huduma kwa mazuwaru, tambua kuwa maukibu ya Ummul-Banina (a.s) katika chuo kikuu cha Al-Ameed, imezowea kutoa huduma tofauti kwa mazuwaru katika kila msimu wa ziara ya Arubainiyya, ni moja ya vituo vinavyo pitiwa na mazuwaru wanaotumia barabara ya (Najafu – Karbala)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: