Maukibu (2328) zinashiriki kuhudumia mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Mkoa wa Baabil ni moja ya vituo muhimu vya watu wanaokwenda Karbala kutoka mkoa wa Diwaniyya na Waasit pamoja na Bagdad wilaya ya Musayyib, kwa ajili ya kuhakikisha wanatoa huduma nzuri kwa mazuwaru wanaopita katika mkoa huo, mawakibu za kutoa huduma zinafanya kazi kwa bidii, zinagawa chakula na kutoa huduma za afya na zinginezo, kazi hizo zitaendelea hadi utakapoisha msimu wa ziara, jumla ya maukibu (2328) zimesambaa kwenye barabara zote zinazo tumiwa na mazuwaru.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya katika Ataba mbili takatifu bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan, akaongeza kuwa: “Maukibu hizo ni zile zilizo sajiliwa rasmi na kitengo, bado kuna makumi ya Husseiniyya na nyumba za watu pamoja na maukibu zisizo sajiliwa zimefungua milango kwa mazuwaru tangu siku ya kwanza na kuwapa huduma mbalimbali ndani ya eneo la mkoa huu”.

Akafafanua kuwa: “Kuna maukibu (243) zitashirikiana na maukibu za mikoa mingine kuhudumia mazuwaru katika mkoa wa Karbala na kwenye barabara zinazo elekea huko”.

Akaongeza kuwa: “Maukibu hizi haziishii kutoa huduma ya chukula pekeyake, bali zinatoa huduma za afya pia kutokana na janga la virusi vya Korona, sambamba na kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama. Baada ya kukatika misafara ya mazuwaru katika mkoa huu, watumishi wa maukibu hizo watakwenda Karbala kufanya ziara na kupata utukufu mara mbili, utukufu wa kutoa huduma kwa mazuwaru na kufanya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: