Maukibu ya Ataba mbili tukufu ni kituo cha kwanza kinacho toa huduma kwa mazuwaru katika barabara ya Najafu – Karbala.

Maoni katika picha
Maukibu ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ni miongoni mwa vituo vya kwanza anavyo pitia zaairu anayetoka Najafu kwenda kibla ya watu huru Karbala takatifu kufanya ziara ya Arubaini.

Maukibu inatoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru, ikiwa ni pamoja na sehemu ya kupumzika, chakula na vinywaji katika nyakazi zote tatu, pamoja na huduma za afya sambamba na kugawa barakoa na soksi za mikononi, halafu muda wote wanapuliza dawa za kuuwa bakteria, huku watumishi wake wakifanyiwa vipimo kila wakati.

Huduma zinazo tolewa siohizo pekeake, sekta ya Dini, utamaduni na elimu zina nafasi kubwa katika huduma zinazo tolewa na maukibu hiyo, kwenye kipindi hiki cha Arubainiyya, kwani huzingatiwa kuwa mradi mkubwa wa tablighi na hauza ya Najafu.

Maukibu inahuduma zingine pia, kama vile kuelekeza waliopotea, sehemu ya kuswalia na ufundishaji wa usomaji sahihi wa Quráni tukufu.

Kumbuka kuwa sehemu ilipo maukibu hii, palikua na maukibu ikituo huduma kwa siri zamani –wakati wa utawala uliopita- wahudumu wa kipindi hicho walipata mateso makubwa, lakini baada ya kuanguka utawala ule na kurudi maadhimisho ya Husseiniyya ndipo maukibu ikaamua kufanya sehemu hii kuwa kituo chake, baada ya kukubaliwa fikra ya kuanzisha maukibu ya kuhudumia mazuwaru kwa jina la (Maukibu ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya), maukibu inafanya kazi kubwa kutokana na ufadhili wa Ataba hizo, kila mwaka hupokea makumi kwa maelfu ya mazuwaru na hugawa maelfu ya sahani za chakula, maukibu hii inatembelewa na mazuwaru wengi zaidi kutokana na ubora wa huduma zake na kwa kuwa ipo chini ya sehemu mbili takatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: