Kwa lugha ya kiengereza: Kitengo cha habari cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendesha kipindi cha (Salam kutoka peponi) kufanya ziara ya Arubaini kwa niaba

Maoni katika picha
Kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimeanzisha kipindi cha mubashara kwa lugha ya kiengereza katika ziara ya Arubaini kwa jina la (Salamu kutoka peponi) kinacho lenga kufanya ziara kwa niaba ya waumini wa kigeni walioshindwa kuja Karbala kufanya ziara ya Arubaini mwaka huu.

Makamo rais wa kitengo cha habari Ustadh Muhammad Asadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Lengo la kuanzishwa kipindi hiki kwa lugha ya kiengereza ni kwa ajili ya kufanya ziara kwa niaba ya mazuwaru wa kigeni, walioshindwa kuja Karbala kufanya ziara katika kipindi hiki cha msimu wa Arubaini”.

Akaongeza kuwa: “Tumetumia mfumo wa matangazo ya mubashara unaorushwa na chanel mbalimbali, hadi sasa kuna jumla ya chanel tano zinazo rusha matangazo ya mubashara kwa lugha ya kiengereza, na tumefanya mawasiliano na mitandoa nane ya kijamii ambayo inataka kushiriki katika kurusha matangazo ya moja kwa moja (mubashara), hadi sasa kuna nchi (11) za kigeni zinazo pata matangazo haya, kipindi hupokea zaidi ya simu (4000)”.

Kumbuka kuwa kipindi hiki kitaendelea hadi mwezi (20) Safar, siku ya kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s).

Tambua kuwa kipindi hiki hurushwa kila siku kuanzia saa (6:00) usiku, kutokea juu ya paa la haram tukufu ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), simu zinapokelewa kupitia mfumo wa mubashara au kupitia whatsap kwa namba zifuatazo:

009647821611120
009647703788789

Chalel inayopenda kurusha matangazo hayo itumie anuani zifuatazo:

ip tv
rtmp =
rtmp://173.212.209.197:1935/abbas/live

Na masafa ya Satellite:

Satellite: Eutelsat 7A at 7.0 East(W3A)
DOWNLINK:12680.200 H
MOD:DVBS2
QPSK
FEC:5/6
Sr :3250
HD/MPEG-4
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: