Muhimu: Tamko la ufafanuzi wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu, Husseiniyya na Abbasiyya, kimetoa tamko la ufafanuzi jioni ya Jumatatu mwezi (18 Safar 1442h) sawa na tarehe (6 Oktoba 2020m) kuhusu tukio la leo katika mji mtukufu wa Karbala, lifuatalo ni tamko hilo:

Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Mwenyezi Mungu, basi hayo ni katika unyenyekevu wa nyoyo (Al-Hajji/32).

Sio siri kwa waumini juhudi kubwa inayofanywa na vikosi vya ulinzi na usalama kila mwaka kwa kushirikiana na mamlaka za serikali, ili kuufanya msimu wa Arubaini kuwa na picha nzuri zaidi ya kumpa pole Mtume na Ahlulbait wake (a.s), juhudi zinazo akisi tabia njema ya raia watukufu wanao jitolea sana katika njia ya kiongozi wao Imamu Hussein (a.s) ya kurekebisha kila kilicho haribika katika Dini ya babu yake (s.a.w.w).

Imekua kawaida kufanya maombolezo ya Husseiniyya hapa Iraq, katika siku kumi za kwanza za mwezi mtukufu wa Muharam kila mwaka, kila mkoa hufanya maombolezo ya bwana wa mashahidi (a.s) katika maeneo yake, na kipindi cha Arubaini watu wote huja Karbala, mawakibu za kila mkoa hushiriki kwenye maombolezo, ukitoa maukibu za Karbala tukufu, ambazo hufanya maombolezo siku kumi za kwanza katika mwezi wa Muharam, na katika msimu wa Arubaini hutoa huduma kwa maukibu za mikoani kama wageni wao.

Kila mtu anajua kuwa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu, tangu kuanzishwa kwake katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya kazi kubwa ya kurahisisha ushiriki wa kila mtu anaetaka kushiriki, kinaratibu mambo yafuatayo:




    • 1- Huduma: Kinasajili maukibu za kutoa huduma na za kuomboleza –zinaongezeka kila mwaka- na hutoa kitambulisho kwa kiongozi wa maukibu na wasaidizi wawili, baada ya kuridhika na uaminifu wa kiongozi. Na miongoni mwa majukumu yake ni kupanga ratiba ya kushiriki kwa mawakibu za kila mkoa katika msimu wa Arubaini.




    • 2- Amani: Hufanya mchakato wa kuthibitisha maukibu kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama vya serikali, hukagua vielelezo vya maukibu na kutoa kibali cha kuruhusu kuingiza mahitaji yao bila usumbufu kwenye vituo vya ukaguzi na getini kwa ajili ya kutoa huduma kwa mazuwaru.




Chini ya makubaliano yaliyofanywa kati ya kitengo na kiongozi wa maukibu, ikiwa ni pamoja na kumtambulisha kila atakae shiriki katika uombolezaji au kutoa huduma, na kujiepusha na kila aina ya ufunjifu wa amani, na kulinda usalama wa waombolezaji na mazuwaru, ukizingatia kuwa matembezi ya maukibu zilizo sajiliwa hufanywa ndani ya mji wa Karbala na huingia katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na uwanja wa katikati yake.

Pamoja na hivyo, maukibu yeyote isiyo sajiliwa haiwezi kuingia katika ratiba ya matembezi ya maukibu katika siku husika, kwa sababu bado haijafuata utaratibu wa kuhakikisha usalama wa waombolezaji na mazuwaru, itazuiliwa kuingia kwa ajili ya kulinda usalama wa wote, kwani maukibu iliyokamilisha masharti huingia bila kukaguliwa, maukibu isiyo sajiliwa halafu ikawa inataka kufanya matembezi ya kuomboleza bila ratiba yeyote ni kuvunja haki ya mawakibu zilizo sajiliwa pamoja na ratiba yao, aidha ni kuvuruga mpangilio wa maombolezo ya Husseiniyya katika msimu wa Arubaini ambao ulimwengu mzima unajifaharisha kwa kuwa na nidhamu nzuri.

Kilicho tokea kwenye maukibu ya jamaa kutoka mkoa wa Dhiqaar walitaka kuingia katika eneo la maombolezo siku ya mwezi 18 Safar 1442h, bila kufuata utaratibu tuliotaja, maukibu yao haijasajiliwa wala hawakuingia kupitia mkoa wao.

Walipo ambiwa kuwa utaratibu na kanuni zilizo wekwa ni kwa ajili ya kulinda usalama wao na usalama wa mazuwaru, na kwa ajili ya nidhamu ya maombolezo ya Husseiniyya, hivyo wanatakiwa kuondoka kwani hawajafuata utaratibu, walikataa, wakataka kuingia kwa nguvu.

Kwakua kufanya hivyo ni kuhatarisha usalama wa mazuwaru na waombolezaji, na kuharibu haiba ya maombolezo ya bwana wa mashahidi na kuchafua muonekano wa maombolezo haya yanayo heshimiwa na kila mtu, ililazimika vikosi vya ulinzi na usalama viwazuwie kutokana na wao kuvunja utaratibu uliowekwa.

Tambua kuwa utaratibu huu unafuatwa na kila mtu, maukibu zote za waombolezaji na za kutoa huduma zinafuata utaratibu huo sawasawa.

Kuhusu kauli mbiu ya kila maukibu, kitengo hakihusiki maadam maukibu inaheshimu manuni na makubaliano waliyo fanya na kitengo.

Maneno yanayo zungumzwa mitaani sio sahihi.

Mwenyezi Mungu atuwezeshe sote kuhuisha alama zake, na kulinda haiba ya maombolezo ya Husseiniyya, pamoja na usalama wa mazuwaru na waombolezaji.. na Mwenyezi Mungu ni mkuu wa kuwafikisha.



Kitengo cha maadhimisho na mawakibu na vikundi vya Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: