Atabatu Abbasiyya tukufu imeka vutuo vinne vya kusambaza maji safi (RO) ujazo wa lita elfu 47/ kwa saa.

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya imeweka vituo vya kusambaza maji safi (RO) kwa mawakibu zinazo hudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), vituo vivyo vinauwezo wa kusambaza ujazo wa lita elfu 47 kwa saa, chini ya usimamizi wa kiwanda cha barafu na shirika la Alkafeel kitengo cha kuzalisha maji ya majumbani kilichopo kwenye kituo cha Saqaa/2 barabara ya (Baabil – Karbala).

Kiongozi wa kiwanda cha barafu katika Atabatu Abbasiyya Mhandisi Ahmadi Amjaad ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kutokana na kuongezeka kiwango cha joto na mahitaji ya maji katika msimu wa ziara, tumefungua vituo vinne (RO) vyenye uwezo wa kusambaza lita elfu 47 kwa saa, kwa ajili ya kuzipatia maji mawakibu zinazo hudumia mazuwaru, tunafuata kanuni zote za afya katika uzalishaji na usambazaji wa maji hayo”.

Akaongeza kuwa: “Kituo kinafanya kazi muda wote, kinasambaza maji kwa kutumia gari zake maalum, au maukibu zinaenda kuchukua maji kwenye vituo moja kwa moja, kazi ya uzalishaji wa maji na usambazaji inafanywa na watu walio bobea katika fani hiyo”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inatumia uwezo wake wote kupokea mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kutoa huduma bora, hii ni moja ya huduma nyingi zinazo tolewa na Ataba tukufu kwa mazuwaru au mawakibu, vipo pia vituo vingine vya kugawa maji safi kwa mazuwaru.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: