Idhaa ya Alkaeel ya mwanamke wa kiislamu inatangaza ziara ya Arubaini kupitia vipindi maalum na matangazo mubashara.

Maoni katika picha
Idhaa ya Alkafeel ya mwanamke wa kiislamu chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu inarusha matangazo ya ziara ya Arubaini, katiba mazingira yanayo endana na utukufu wa ziara hiyo, chini ya hali halisi wanayo ishi wasikilizaji wake ndani na nje ya mkoa wa Karbala, bali hata nje ya Iraq, kwani inarusha matangazo yake pia kupitia masafa maalum inayo rusha matukio ya ziara hii.

Haya yameelezwa na makamo rais wa kitengo cha habari na utamaduni Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri kwenye mtandao wa Alkafeel, akaongeza kuwa: “Kitengo kimeweka mkakati maalum wa kutangaza ziara ya Arubaini, ambao upo chini ya mkakati wa Atabatu Abbasiyya katika sekta ya elimu, utamaduni na muongozo, idhaa ya Alkafeel inatekeleza sehemu ya mkakati huo, imeandaa vipindi vinavyo rusha matukio yaliyo rekodiwa ndani ya muda mfupi uliopita na vipindi vya kurusha matukio mubashara”.

Akafafanua kuwa: “Vipindi vilikua vinahusu, maelekezo, utamaduni na maombolezo ya tukio hili, na namna ya kunufaika na ziara hii na kutambulisha malengo yake kidini, kitamaduni na kijamii, na jinsi ya kumsaidia mwanamke wa kiislamu na familia za wairaq kwa lunga nzuri inayo eleweka kwa urahisi, isiyojenga chuki na ubaguzi, huku vipindi vikipambwa na aya za Quráni pamoja na hadithi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s) zinazo himiza jambo hilo”.

Akamaliza kwa kusema: “Vipindi hivyo pia vilikua na sehemu ya mashindano na mahojiano kuhusu harakati za wanawake zinazo fanywa na watumishi wa Ataba tukufu, vipindi hivyo vitaendelea hadi mwisho wa mwezi huu baada ya kukumbuka kifo cha Mtume (s.a.w.w), tukio la kumbukumbu ya kifo cha mtume lipo ndani ya ratiba ya vipindi vya idhaa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: