Masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu watafanya zaiara ya Arubaini kwa niaba ya kila aliyepata udhuru wa kuja kufanya ziara hiyo mwaka huu

Maoni katika picha
Idara ya masayyid wanaotoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuwa, kesho mwezi ishirini Sarar itafanya ziara maalum ya Imamu Hussein (a.s) pamoja na ziara ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na swala ya rakaa mbili na dua kwa niaba ya watu waliojiandikisha kwenye ukurasa wa ziara kwaniaba uliopo katika mtandao wa Alkafeel, walioshindwa kuja kufanya ziara kutokana na janga hili la virusi vya Korona.

Hayo yamesemwa na kiongozi wa idara hiyo Sayyid Hashim Shami, akaongeza kuwa: “Kutokana na kauli ya Abu Muhammad Hassan Askariy (a.s) isemayo: (Alama za muumini ni tano: swala (rakaa) hamsini na moja, ziara ya Arubaini, kuvaa pete kwanye mkono wa kulia, kuweka paji la uso chini, na kusoma bismilahi kwa sauti), wahudumu wa idara yetu katika Atabatu Abbasiyya tukufu kesho watafanya ziara kwaniaba ya kila mpenzi na mfuasi wa Ahlulbait (a.s) kote duniani, wale ambao umbali umewazuwia kuja Karbala kufanya ziara ya Arubaini katika mazingira haya ya janga la virusi vya Korona, na walio sajili majina yao kwenye ukurasa wa ziara kwaniaba kupitia link ifuatayo: https://alkafeel.net/zyara/”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: