Mwezi ishirini Safar msafara wa mateka ulirudi Karbala

Maoni katika picha
Simama uhuishe huzuni mwezi ishirini Safar… siku hiyo vichwa vilirudishwa kwenye miili yake.

Familia ya Mtume iliyo halalishwa damu yao… katika dini ya watu ambao hata makafiri wako mbali nao.

Katika siku kama ya leo mwaka wa 61 hijiriyya, ilikua ni siku ya Arubaini tangu kufanyika kwa mauwaji ya Karbala, ambayo aliuwawa Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake pamoja na wafuasi wake (r.a).

Vitabu vya historia vinasema kuwa, wakati msafara wa mateka unarudi Madina kutoka Sham, walifika njia panda ya kwenda Iraq na kwenda Hijazi, wakamuambia muongozaji wa njia: tupitishe Karbala.

Mwezi ishirini Safar (ambayo ni siku ya Arubaini) wakafika Karbala, wakazuru kaburi la Imamu Hussein (a.s) na watu wa nyumbani kwake na wafuasi wake na wakafanya vikao vya maombolezo, wakabaki katika hali hiyo kwa siku kadhaa.

Kutoka kwa Atwiyya Aufi anasema: Niondoka na Jaabir bun Abdillahi Answari (r.a) kwenda kuzuru kaburi la Hussein (a.s), tulipofika Karbala Jaabir akasogea pembeni ya mto wa Furaat, akaoga halafu akajifunga shuka na nyingine akajifunika, kisha akajipaka marashi, kila hatua aliyo piga akawa anamtaja Mwenyezi Mungu mtukufu. Hadi alipo karibia kaburi akasema: nishikishe kaburi, nikamshikisha. Akaanguka juu ya kaburi na kuzimia, nikamwagia maji kidogo akazinduka.

Baada ya kuzinduka akasema: Yaa Hussein (mara tatu). Kisha akasema: Mpenzi hawezi kumjibu mpenzi wake, haiwezekani ukajibu wakati wamekata koo lako, na wametenganisha kichwa na muili wako, nashuhudia wewe ni mtoto wa Mtume wa mwisho, mtoto wa bwana wa waumini, mtoto wa mchamungu na muongozaji wa uongofu, wewe ni mtu wa tano katika watu wa shuka (as-habul-kisaa), mtoto wa bwana wa uongofu, mtoto wa Fatuma mbora wa wanawake. Kwa nini usiwe hivi wakati ulikua unalishwa na mkono wa bwana wa mitume, umelelewa na miguu ya wachamungu, umenyonya maziwa ya Imani yaliyojaa uislamu, ulikua bora katika uhai na uko bora baada ya kufa. Hakika nyoyo za waumini hazina furaha baada yako, amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako na rehma zake, nashuhudia hakika umepita njia aliyo pita ndugu yako Yahya bun Zakariyya.

Kisha akaangalia pembeni ya kaburi na akasema: Amani iwe juu yenu enyi nyoyo mlio jitolea kwa ajili ya Hussein (a.s), nashuhudia kuwa mlisimamisha swala na mlitoa zaka, mliamrisha mema na kukataza mabaya, mlipigana jihadi na kumuabudu Mwenyezi Mungu hadi milipofikwa na kifo.

Naapa kwa yule ambae alimtuma Muhammad kuwa Mtume, tumeshirikiana na nyie katika mliyopitia. Atwiyya akasema: Hapana. Kwa nini hatukutembea jangwani pamoja nao, na watu wamewauwa na kutenganisha vichwa na miili yao, watoto wao wamekua mawatima, na wake zao wamekua wajane, sisi hatuja panda mlima wala kupigwa panga!!?

Jaabir akasema: Ewe Atwiyya, mimi nilimsikia kipenzi wangu Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) anasema: (Atakaependa watu atafufuliwa pamoja nao, na atakaependa vitendo vya watu atashirikishwa katika vitendo vyao). Naapa kwa aliyemtuma Muhammad kwa haki, hakika niya yangu iko swa na nia ya wafuasi wa Hussein (a.s) katika mambo waliyo pitia.

Atwiyya akasema: Tulipokua hapo mara nikaona msafara unatokea upande wa Sham. Nikasema: Ewe Jaabir, kuna msafara unakuja kutoka upande wa Sham, Jaabir akamuambia kijana wake, ufuatilie msafara huo na unipe taarifa, kama ni katika watu wa Omari bun Saadi rudi haraka tuangalie sehemu ya kujihifadhi, na kama ukiwa ni msafara wa Zainul-Aabidina (a.s) utakua huru kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mtukufu.

Akasema: Yule kijana akaenda, mara akarudi haraka kwa Jaabir huku akisema: Ewe Jaabir, simama upokee haram ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w). Huyu hapa Zainul-Aabidina (a.s) amekuja na shangazi yake pamoja na dada zake. Jaabir akasimama akawa anatembea miguu chini kichwa wazi, hadi alipo mkaribia Zainul-Aabidina (a.s), Imamu (a.s) akasema: Wewe ni Jaabir? Akasema: Ndio, ewe mtoto wa Mtume wa Mwenyezi Mungu. Akasema: Ewe Jaabir, Hapa ndio walipouwawa watu wetu, na kuchinjwa watoto wetu, na kutekwa wanawake wetu, na kuchomwa hema zetu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: