Idara ya masayyid imetaja kazi inazofanya katika kuwahudumia mazuwaru na mawakibu za kuomboleza

Maoni katika picha
Idara ya masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya tukufu imetaja kazi walizo fanya katika kutekeleza majukumu waliyo pewa kama moja ya vitengo vya Ataba tukufu katika kuhudumia mazuwaru wa Arubaini na mawakibu za kuomboleza, utawakuta wamesambaa kila sehemu ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kiongozi wa idara hiyo Sayyid Hashim Shami ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Idara ya masayyid inamchango mkubwa katika kusaidia vitengo vingine kwenye ziara ya Arubaini, wanafanya kazi muda wote katika kila sehemu ya haram tukufu, wanaongoza mazuwaru kwenye maeneo mbalimbali wanayo kusudia kwenda, wanajibu maswali ya mazuwaru, wanaongoza watembeaji ndani ya haram na kuzuwia misongamano”.

Akaongeza kuwa: “Masayyid wanasafisha haram tukufu na miswala (mazulia), wanapanga misahafu na vitabu vya ziara kwenye kabati zake”.

Akabainisha kuwa: “Wanapangilia uingiaji na utokaji wa mawakibu za kuomboleza kwa namna ambayo haziingiliani na harakati za mazuwaru, pamoja na kuwasomea ziara tukufu baadhi ya watu wenye umri mkubwa, aidha kuna kundi la masayyid wamekwenda kuhudumia mazuwaru kwenye migahawa ya Atabatu Abbasiyya tukufu iliyopo nje ya haram kwenye barabara zinazo elekea Karbala”.

Akamaliza kwa kusema: “Miongoni mwa kazi zinazo fanywa na masayyid ni kufanya ziara kwaniaba na kuwaombea dua mazuwaru watukufu kwa ajili ya kila mtu aliyeshindwa kuja katika malalo takatifu, watahitimisha kwa kufanya ziara maalum ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: