Jumla ya maukibu (32,000) zimeshiriki katika ziara ya Arubaini (20) kati ya hizo zimetoka nchi za kiarabu na kiajemi

Maoni katika picha
Kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya hapa Iraq na katika ulimwengu wa kiislamu chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimesema kuwa: Idadi ya maukibu za -kutoa huduma na kuomboleza- zilizo shiriki katika ziara ya Arubaini mwaka huu zimefika (32,000), zilizo sajiliwa rasmi. Miongoni mwa hizo, maukibu (20) kutoka nchi za kiarabu na kiajemi, nchi hizo ni: Pakistani, India, Saudia, Kuwait, Lebanon, Naijeria, Uingereza.

Kwa mujibu wa maelezo ya bwana Riyaadh Ni’mah Salmaan rais wa kitengo, aliyotoa kwenye mtandao wa Alkafeel. Akabainisha kuwa: “Maukibu za kuomboleza za (zanjiil na matam) zilikua (973) kutoka mikoa tofauti ya Iraq, maukibu za zanjiil zilikua (287) na maukibu za matam zilikua (686), maukibu hizo zilishiriki katika kuomboleza kwa muda wa siku nne”.

Akaongeza kuwa: “Maukibu zilizo shiriki kutoa huduma kwa mazuwaru, kuanzia kituo cha mbali kabisa zinakoanzia misafara ya mazuwaru hadi kufika Karbala, zimefika (32,027), zimetoa huduma ya chakula, vinywaji, sehemu ya kupumzika na kulala pamoja na huduma zingine nyingi, bila kusahau huduma za afya, ukizingatia kuwa tupo katika kipindi cha janga la maambukizi ya virusi vya Korona, maukibu (10,350) ndio ambazo zimetoa huduma ndani ya mipaka ya mkoa wa Karbala, ikiwa ni pamoja na mawakibu za mkoa huu (Karbala) na mikoa mingine, bila kusahau kuna maukiu, huseiniyya na nyumba za watu mamia kwa mamia zimehudumia mazuwaru bila kusajiliwa na kitengo chetu”.

Akasema: “Maukibu za kiarabu na kiajemi mwaka huu zimetosheka na kuomboleza tu, kutokana na mazingira ya kuruhusiwa kwao kuingia Iraq, kwa sababu ya janga la Korona, aidha walifika wakiwa wamechelewa”.

Akafafanua kuwa: “Kitengo kilihakiki maukibu hizo mapema na kikatoa vitambulisho kwa viongozi wao, jambo ambalo ndio sharti la kushiriki kwa maukibu ya kuomboleza au kutoa huduma, kitengo kiliweka watumishi wake na wasaidizi wao wanaofanya kazi kwa kujitolea kila sehemu, kwa ajili ya kuratibu na kuongoza matembezi ya mawakibu hizo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: