Atabatu Abbasiyya tukufu imesema kuwa: Zaidi ya watu milioni 14 wamefanya ziara ya Arubaini mwaka huu 1442h.

Maoni katika picha
Baada ya Adhuhuri ya leo, Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa tamko rasmi kuhusu idadi ya mazuwaru waliosajiliwa na mfumo wa kuhesabu watu kielektronik kuanzia mwezi (9) Safar hadi mcha wa mwezi (20) Safar 1442h, imefika milioni kumi na nne laki tano hamsini na tatu elfu na mia tatu na nane (14,553,308). Hao ni wale walio ingia kupitia barabara tano kuu, ambazo ni: (Bagdad – Karbala, Najafu – Karbala, Baabil – Karbala, Husseiniyya – Karbala na Huru Karbala).

Ifuatayo ni nakala ya tamko:

Idadi ya mazuwaru kwa mujibu wa mfumo wa kuhesabu watu kielektronik katika Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya Karbala takatifu katika Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) mwaka huu 1442h.

Amani iwe juu ya Hussein na Ali bun Hussein na watoto wa Hussein na wafuasi wa Hussein, amani iwe juu yako ewe Abulfadhil Abbasi.

Tunatuma salam za rambirambi kwa Imamu wetu Hujjat bun Hassan (f.a) na maraajii watukufu pamoja na ulimwengu wa kiislamu kwa ujumla, hususan Iraq ya Mitume, mawasii na mawalii, katika kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu ailinde miji ya waislamu kutokana na kila ubaya, na awarejesha mazuwaru wa Abu Abdillahi Hussein (a.s) katika miji yao wakiwa salama na faida ya kukubaliwa ibada zao.

Kama kawaida yetu kwa zaidi ya karne (13) mji mtukufu wa Karbala umekua ukipokea mazuwaru wa bwana wa mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ziara ya Arubainiyya, mwaka huu 1442h Atabatu Abbasiyya imepata utukufu wa kuwapokea na kuwahudumia mazuwaru hao, wamepewa huduma za aina tofauti, ikiwa ni pamoja na huduma ya kuwahesabu kwa kutumia mfumo wa kielektronik, wale walio ingia Karbala kupitia barabara kuu, huduma hiyo imesimamiwa na idara ya mawasiliano katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mwaka wa tano mfululizo, na kuthibitisha taarifa zake kupitia watumishi wengine katika mji wa Karbala wa kituo cha taaluma tafiti na takwimu Alkafeel.

Idadi ya mazuwaru waliosajiliwa kwenye mfumo wa kuhesabu watu kielektronik uliofungwa kwenye barabara kuu tano za (Bagdad – Karbala, Najafu – Karbala, Baabil – Karbala, Husseiniyya – Karbala na Huru – Karbala) imefika milioni kumi na nne laki tano hamsini na tatu elfu na mia tatu na nane (14,553,308), kuanzia mwezi (9) Safar hadi mchana wa mwezi (20) safar 1442h. Tambua kuwa idadi ya mazuwaru wa mwaka jana 1441h, ilikua milioni kumi na tano laki mbili na ishirini na tisa elfu mia tisa na hamsini na tano (15,229,955), na mwaka juzi 1440h ilikua milioni kumi na tano laki tatu na ishirini na mbili elfu mia tisa na arubaini na tisa (15,322,949), na katika mwaka 1439h, ilikua milioni kumi na tatu laki nane na sabini na nne eflu mia nane na kumi na nane (13,874,818).

Tunamuomba Mwenyezi Mungu atukubalie ibada zetu na atuwezeshe kufanya mambo anayo yapenda na kuyaridhia hakika yeye ni mwingi wa kusikia mwingi wa kujibu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: