Atabatu Abbasiyya inapuliza dawa mfululizo katika majengo yanayo tumika katika kuhudumia mazuwaru wa Arubaini

Maoni katika picha
Katika mkakati wa afya ulio andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwenye ziara ya Arubaoni, kuna kipengele cha kupuliza dawa kwenye majengo yote yanayotoa huduma chini yake yaliyopo pande kuu tatu za mkoa mtukufu wa Karbala.

Upulizaji huo wa dawa pamoja na mambo mengine ya afya ni kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona, na kulinda usalama wa mazuwaru, ambao ni utukufu kwetu kuwahudumia, tahadhari za kujikinga na maambukizi zinafanywa katika hali ya juu kwa kutumia vifaa vyenye ubora mkubwa kutoka shirika la Khairul-Juud.

Kutokana na kuwa na wageni wengi katika majengo yanayo toa huduma kwa mazuwaru, idara ya madaktari inasimamia shughuli za uchukuaji wa tahadhari za kujikinga na maambukizi, kuna kikosi maalum kutoka kitenge cha vijana wa Alkafeel idara ya watoto na makuzi ambacho kimegawanyika sehemu mbili: sehemu ya kwanza wapo nje ya kila jengo linalo toa huduma, jukumu lao ni kupuliza dawa kwa mazuwaru wanaopita mbele ya jengo, na sehemu ya pili wanapulia dawa kwa mazuwaru wanao ingia ndani ya jengo hilo.

Kwa upande mwingine tumeweka mtambo wa kupuliza dawa kwa kila mtu anaeingia katika jengo linalo tumika kutoa huduma, kama vile: (mgahawa wa nje – maukibu Ummul-Banina (a.s) katika chuo kikuu cha Al-Ameed – jengo la Alqami – jengo la Kuleini), mtambo mmoja unapuliza watu wanao ingia na mwingine wanaotoka, kazi hiyo imefanywa na kitengo cha usimamizi wa kihandisi, dawa zinazo tumika zimethibitishwa na mamlaka husika hazina madhara yeyote kwa binaadamu.

Pamoja na hayo kuna upulizaji wa dawa muda wote katika sehemu zote za jengo, kama vile: sehemu ya kupumzika, sehemu ya chakula, sehemu za kulala (vyumbani), vyooni, bustanini na sehemu zingine.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua tahadhari mbalimbali za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya kujikinga na maambukizi kama inavyo tolewa na mamlaka za afya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: