Kwa ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Shirika la mawasiliano Alkafeel limefungua vituo mia mbili vya kupiga simu bure kwa mazuwaru

Maoni katika picha
Chini ya ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu, shirika la mawasiliano Alkafeel limefungua vituo (200) vya kupiga simu bure kwenda mitandao yote ndani na nje ya nchi, vituo hivyo vimefunguliwa sehemu tofauti katika barabara zinazo tumiwa na mazuwaru wa Arubaini kuelekea Karbala, pamoja na kwenye vituo vya waliopotea ndani ya mkoa wa Karbala na Najafu pamoja na kwenye barabara zinazo kwenda kwenye mikoa hiyo.

Asilimia kubwa ya vituo hivyo vilianza kufanya kazi tangu siku za kwanza za ziara hii, kwenye vituo vya kusaidia walio potea, vituo vya utambulisho na vituo maalum, wanatumia simu za mezani, kituo kimetumia ujuzi mkubwa kuhakikisha simu zinasikika vizuri bila kukatika katika, au kuwa na sauti mbaya jambo ambalo hutokea kutokana na muingiliano wa mawasiliano, huduma hii imefurahiwa sana na mazuwaru, kwani imewawezesha kuongea na familia zao au marafiki zao, pia imewasaidia kuwapata waliopotea kwa urahisi.

Rais wa kituo cha kusaidia waliopotea bwana Haidari Muhyi-Dini amesema kuwa, huduma ya kupiga simu bure inayo tolewa na shirika la mawasiliano Alkafeel, ni sawa na uti wa mgongo katika maradi wa kusaidia na kuongoza walio potea, kwani inarahisisha kuwasiliana kati ya kituo na kituo pia inasaidia kumpata aliyepotea kwa urahisi, akasifu ushirikiano mkubwa uliopo kati yao tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo hadi leo, na ushirikiano huo huongezeka zaidi katika ziara ya Arubaini kwa kua na mamia ya vituo vinavyo toa huduma ya kupiga simu bure katika barabara zinazo tumiwa na mazuwaru hadi katika ardhi ya Karbala.

Kumbuka kuwa shirika la mawasiliano la Alkafeel lilianzishwa kwa ajili ya kusaidia upigaji wa simu bure kwa mazuwaru wakati wa matukio ya kidini, huduma hiyo imeongezeka baada ya kupata ufadhili wa Atabatu Abbasiyya tukufu, hakika mazuwaru wana haja kubwa ya huduma hiyo wakati wa msimu wa ziara, huwa kuna msongamano mkubwa wa mazuwaru wanaotaka kuwapigia simu jamaa zao, shirika huwezesha mawasiliano kati ya zaairu na jamaa zake ndani au nje ya nchi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: