Kituo cha vijana wa Alkafeel kinataja namna kilivyo kubalika katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kituo cha kijana wa Alkafeel kilipata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru wakati wa ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s), kutokana na kuwa na idadi kubwa ya vitengo vya elimu na utamaduni, kilikua na jumla ya vituo (16) vilivyokua vikitoa elimu mbalimbali.

Kiongozi wa idara ya mahusiano ya vyuo vikuu na shule Ustadh Maahir Khalidi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Tulitegemea mfumo wa uandishi wa kielektronik kwa zaairu, kituo hicho kilifunguliwa mwezi (12) Safar na kufungwa mwezi (20) Safar, kwa lengo la kujua idadi ya mazuwaru na kiwango cha kukubalika kwa vitengo vya kituo”.

Akafafanua: “Katika mwaka wa kwanza kituo kilipata mazuwaru (3750) kwa mujibu wa takwimu tulizo nazo, kituo cha Sanaa na uigizaji wa tukio la Twalu kimepata muitikio mkubwa, kuna viwango tofauti kati ya kituo na kingine, kwa mfano kituo na kujenga uwezo, maendeleo ya binaadamu na vipaji vya vijana”.

Akaongeza kuwa: “Hali kadhalika ofisi ya (Soma kitabu na uchukue zawadi ya nafsi yako) imepata muitikio mkubwa kutoka kwa vijana, pamoja na igizo lililofanywa katika kituo hicho kwa kushirikiana na jumuiya ya Skaut ya Alkafeel, vipande vya igizo vilifanywa asubuhi na jioni, pamoja na zaairu wa chama cha kitamaduni cha Alqamaru na kitengo cha kuishi kwa amani”.

Akasisitiza kuwa: “Hua tunakua na ujumbe katika kituo cha utamaduni kila mwaka kwa lugha tofauti, mwaka huu tumekua na ujumbe kwa lugha ya Kiengereza na Kifaransa, miaka ijayo tutajitahidi kuongeza lugha zingine, hali kadhalika kuna vituo vingine vilivyo funguliwa kwenye barabara zinazo ingia katika mji mtukufu wa Karbala”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: