Watumishi wa kitengo kinacho hudumia uwanja wa katikati ya haram mbili wanafanya usafi baada ya kumaliza msimu wa ziara ya Arubaini.

Maoni katika picha
Watumishi wa kitengo kinacho hudumia uwanja wa kazikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya wanafanya usafi: wanasafisha uwanja wa katikati ya haram mbili na barabra zinazo elekea kwenye uwanja huo, wamezowea kufanya hivyo kila mwaka baada ya kuisha kwa msimu wa ziara ya Arubaini.

Rais wa kitengo hicho Ustadh Naafii Mussawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kama kawaida baada ya kumaliza msimu wa Arubaini watumishi wa kitengo chetu hufanya usafi unao husisha uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu na barabara zinazo elekea eneo hilo”.

Akaongeza kuwa: “Asilimia kubwa ya watumishi wa kitengo hicho wanashiriki katika kazi hiyo, wamemaliza haraka kufanya usafi katika maeneo tuliyo taja”.

Akasema: “Wamefanya kazi mfululizo hadi wakamaliza kuondo uchafu wote kwenye barabara zinazo zunguka uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu, hadi kwenye milango ya mji mkongwe pamoja na kupiga deki”.

Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, kimefanya kazi kubwa wakati wa ziara ya Arubainiyya, katika kuhudumia mazuwaru wa bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), waliokuja kwa mamilioni katika ardhi ya Karbala na kupita katika uwanja wa katikati ya haram mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: