Haya ndio yaliyofanywa na idara ya kusimamia haram tukufu katika ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kazi kubwa imefanywa na watumishi wa idara ya kusimamia haram tukufu ya Atabatu Abbasiyya wakati wa ziara ya Arubainiyya, wamefanya kazi ya uratibu, ulinzi na afya.

Kiongozi wa idara hiyo bwana Nizaar Ghina Khaliil ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Tuliratibu uingiaji wa mazuwaru ndani ya haram tukufu wakati wa ziara, kwa ajili ya kurahisisha uingiaji wao, haram tuliigawa sehemu mbili, sehemu ya watu wanao ingia na sehemu ya watu wanaotoka, ili kupunguza msongamano ndani ya haram”.

Akaongeza kuwa: “Tuliendelea na kazi ya kupuliza dawa hata ilipo ongezeka idadi ya mazuwaru, hatukusimama kusafisha ukuta, paa, mapambo na maraya sambamba na kupuliza marashi”.

Akaendelea kusema: “Kulikua na ushirikiano mkubwa sana kati yetu na vitengo vingine pamoja na idara tofauti za Ataba tukufu, miongoni mwake kitengo cha kulinda nidham, idara ya mawasiliano kwa ajili ya maswala ya ulinzi wa amani, idara ya masayyid kwa ajili ya kutoa huduma na kufanya usafi”.

Akasema: “Tulitenga sehemu maalum za kutoa huduma za afya ndani ya haram tukufu, kwa kushirikiana na idara ya madaktari, na tukaweka vifaa tiba vyote vya lazima”.

Akasema kuwa: “Tulipokea idadi kubwa ya wafanyakazi wa kujitolea, ambao tuligawa muda wao wa kazi katika zamu tatu (asubuhi, mchana na jioni), walikua na uzowefu wa kutoa huduma katika ziara za milionea, wamefanya kazi saa (24) kila siku.

Akasema: “Baada ya kumaliza ziara tumesafisha dirisha takatifu kwa kutumia vifaa maalum”.

Kumbuka kuwa idara ya usimamizi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya, ni miongoni mwa idara za kutoa huduma ambazo hufanya kazi kubwa katika siku za ziara kubwa hasa kwenye ziara ya Arubainiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: