Kwa ushiriki wa maustadhi 226: Mradi wa kufundisha kisomo sahihi kwa mazuwaru unatoa taarifa ya mafanikio yake

Maoni katika picha
Mradi wa kufundisha kisomo sahihi kwa mazuwaru, unaosimamiwa na Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika ziara ya Arubainiyya, imepata muitikio mkubwa kutoka kwa mazuwaru walio tembea masafa marefu kwa mikuu, hadi kufika katika Kibla ya watu huru Karbala na kufanya ibada ya ziara ya Arubaini.

Mkuu wa Maahadi ya Quráni tukufu Shekh Jawadi Nasrawi ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kuwa: “Tumefanya mradi huu mtukufu kwa mwaka wa nane mfululizo chani ya utekelezaji mkubwa wa kanuni za afya, kutokana na kuwepo kwa janga la maambukizi ya virusi vya Korona, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu, na kama tulivyo zowea kila mwaka, tumepata muitikio mkubwa kila mahala, tumefundisha usomaji sahihi wa surat Al-Faatihah na sura fupifupi kwa mazuwaru, wanaokuja Karbala kufanya ziara ya Arubaini, wanufaika wakubwa walikua ni wasiojua kusoma na watoto wadogo”.

Akaongeza kuwa: “Mwaka huu tulikua na walimu (226) tuliwagawa kwenye vituo 44, vilivyo kuwepo Muthanna, Baabil, Bagdad, Najafu na ndani ya mji wa Karbala na wilaya ya Hindiyya, kwenye barabara tofauti zinazo tumiwa na mazuwaru kwenye mikoa hiyo kuelekea Karbala, katika jumla ya barabara (19)”.

Kuhusu uendeshaji wa mradi huu, Nasrawi amesisitiza kuwa: “Mwaka huu tulikusudia kuendelea na mradi huu pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali, kwa baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s), tumefanikiwa kufundisha kisomo sahihi cha surat Al-Faatihah pamoja na sura fupifupi kwa maelfu ya mazuwaru”.

Kumbuka kuwa tumefanya mradi huu kwa mwaka wa nane mfulumizo, baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika miaka saba iliyo pita.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: