Mwezi 23 Safar kilitokea kifo cha bibi Fatuma binti Asadi (a.s)

Maoni katika picha
Bibi Fatuma bint Asadi bun Hashim bun Abdumanafi, mama wa kiongozi wa waumini Ali (a.s) na mke wa Abu Twalib (a.s), alizaliwa kabla ya Mtume kuhama Maka (hijira) kwa miaka hamsini na tano takriban, na akafa mwezi ishirini na tatu Safar mwaka wa nne hijiriyya katika mji wa Madina.

Mwanzoni mwa uhai wake alikua katika mila (Dini) ya nabii Idrahim (a.s), alikua mtu wa kumi na moja kuingia katika uislamu, naye ni mwanamke wa kwanza kumkubali Mtume (s.a.w.w) katika mji wa Maka baada ya bi Khadija (a.s).

Baada ya kifo chake katika mwaka wa nne Hijiriyya, Mtume (s.a.w.w) alimvisha sanda kwa kanzu yake, halafu akasema: (Jibrilu (a.s) ameniambia kuwa huyu ni katika watu wa peponi, na ameniambia kuwa Mwenyezi Mungu ameamrisha malaika elfu sabini wamswalie) kisha Mtume (s.a.w.w) akamswalia na akashindikiza jeneza lake hadi katika makaburi ya Baqii, na akamzika hapo.

Kaburi lake takatifu lipo Baqii karibu na makaburi ya Maimamu wa Ahlulbait (a.s), ilivunjwa kubba yake pamoja na kubba za makaburi mengine matakatifu.

Bibi Fatuma bint Asadi (a.s) aliishi pamoja na Abu Twalib (a.s), alitekeleza vizuri majukumu ya kuendesha familia yake, kwa subira, ukweli na ikhlasi, pamoja na mapenzi na Imani kubwa, akamzalia watoto wa kiume na wa kike, ambao ni: Twalibu, Aqiil, Jafari, Ali (a.s), Ummu Haani na Jamanah.

Miongoni mwa sifa za bibi Fatuma bint Asadi (a.s), anaziara maalum tofauti na mama wengine wa maasumina, ispokua Swidiiqatu Zaharaa (a.s) na bibi Narjisi (a.s), miongoni mwa yanayo onyesha ukubwa wa heshima na utukufu wake ni maneno adhim.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: