Zaidi ya mazuwaru laki moja wamefanyiwa ziara ya Arubaini kwaniaba

Maoni katika picha
Idara ya taaluma za mitandao chini ya kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuwa dirisha la ziara kwa niaba lililopo katika mtandao wa kimataifa wa Alkafeel, limepokea na kufanya ziara ya Arubaini kwa niaba ya zaidi ya mazuwaru laki moja, kutoka nchi mbalimbali duniani, kupitia mitandao yake ya (Kiarabu – Kiengereza – Kifarsi – Kituruki – Ki-Urdu – Kifaransa – Kiswahili – Kijerumani).

Ustadh Haidari Twalibu Abdul-Amiir kiongozi wa idara hiyo amesema kuwa: “Kutokana na mazingira ambayo ulimwengu unapitia kwa sasa na kwa namna ya pekee taifa la Iraq, kufuatia kuwepo kwa janga la virusi vya Korona lililo sababisha idadi kubwa ya watu kushindwa kuja kufanya ziara kwenye malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ukurasa huu umeshuhudia watu wengi waliojisajili kutoka nchi tofauti duniani, hivyo tuliweka ratiba maalum ya kufanyia ziara kwa niaba”.

Akafafanua kuwa: “Ndugu zetu masayyid wanaofanya kazi katika Atabatu Abbasiyya walichukua jukumu la kufanya ziara hizo ndani ya malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akaendelea kusema: “Kulikuwa na muda mrefu wa kutangaza ziara hii, ili kutoa nafasi ya watu kujisajili, asilimia kubwa ya watu waliojisajili wametoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistani, Urusi, Marekani, Uingereza, India, Saudia, Swiden, Kanada, Kuait, Malezia, Australia, Aljeria, Baharaini, Misri, Ujerumani, Island, Namsa, Yunani, Holandi, Tunisia, Denmak, Norway, Gana, Yemen, Ubelgiji, Moroko, Afughanistani, Oman, Ekwado, Brazili, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Adharbijani, Italia, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Qabrus, Finland, China, Ailand, Honkon, Japani, Imarat, Sudani).

Akamaliza kwa kusema: “Sasa hivi tunajiandaa kwa ajili ya kufanya ziara kwa niaba wakati wa kumbukumbu ya kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w) mwezi (28) Safar, kupitia dirisha hilihili katika mtandao wa Alkafeel, na itafanywa sawa na ziara iliyopita kutokana na mazingira ya sasa, ambayo yanasababisha idadi kubwa ya watu washindwe kuja kufanya ziara”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: