Zaidi ya mawakala wa vyombo vya habari 63 wameshiriki kutangaza matukio ya ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuwa; Zaidi ya mawakala wa vyombo vya habari stini na tatu vya kitaifa na kimataifa wameshiriki kutangaza matukio ya ziara ya Arubaini mwaka huu.

Muhammad Asadi makamo rais wa kitengo cha habari katika taarifa aliyotoa kwa mtandao wa kimataifa Alkafeel amesema kuwa: “Zaidi ya mawakala stini na tatu wa vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa, ambavyo ni magazeti, redio na luninga pamoja na waandishi mbalimbali, wameshiriki kutangaza matukio ya ziara ya Arubaini katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya pamoja na kwenye uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Ratiba ya utangazaji imetekelezwa chini ya kanuni zilizo undwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya zilizo saidia kuonyesha picha halisi ya ziara ya Arubaini, sambamba na kuweka vitendea kazi vyote vilivyo hitajika katika kutekeleza jukumu la urushaji wa matukio ya ziara hiyo”.

Akasisitiza kuwa: “Kutokana na upekee wa ziara hii kwa sababu ya kuwepo janga la virusi vya Korona, jambo hilo halikuzuwia utangazaji wa ziara hii katika vyombo vya habari vya ndani na nje ya Iraq, vikiwemo vyombo vya habari ambavyo vimeshiriki kwa mara ya kwanza kutangaza tukio hili muhimu la kimataifa”.

Akabainisha kuwa: “Vyombo hivyo vilianza mara moja kutangaza baada ya kuwasiri Karbala, na vimeweza kuonyesha picha halisi ya ziara hiyo”.

Akafafanua kuwa: “Kitengo cha habari kiliweka utaratibu maalum wa kutekeleza majukumu yake, ikiwa ni pamoja na kuweka kanuni kwa kila chombo cha habari kilichataka kurusha matangazo hayo, kilitakiwa kutuma maombi na kuingizwa kwenye orodha maalum ya waandishi wa habari, kisha walipewa vitambulisho (baji) maalum, jumla ya vitambulisho (189) vilitolewa”.

Asadi akasema kuwa: “Kitengo hiki kupitia kituo cha uzalishaji wa vipindi Alkafeel, kiliandaa masafa maalum ya kurusha matangazo bure, kwa ubora wa hali ya juu (clean), kupitia masafa hiyo tumefanikiwa kufikisha sauti ya ziara hii na matukio yake kila sehemu ya dunia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: