Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimeshuhudia kundi kubwa la watu wanaoshindikiza jeneza la mhadhiri wa mimbari ya Husseiniyya Sayyid Jaasim Towirajawi

Maoni katika picha
Kwa huzuni kubwa na masikitiko, Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya baada ya Adhuhuri ya leo (24 Safar 1442h) sawa na tarehe (12 Oktoba 2020m), zimeshuhudia kundi kubwa la watu waliojitokeza kushindikiza muili wa mhadhiri wa mimbari ya Husseiniyya marehemu Sayyid Jaasim Towirajawi, aliye fariki Alfajiri ya jana, amepata umati mkubwa sana wa tutu waliojitekeza kumshindikiza, wakiwemo viongozi wemgi wa dini miongoni mwa wakazi wa Karbala na mazuwaru wake, na wengine wamekuja kutoka miji tofauti kwa ajili ya mazishi yake.

Umati wa washindikizaji umeanzia katika barabara ya Kibla ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi kwenye uwanja wake mtukufu, amefanyiwa ibada ya ziara kwa niaba na zikasomwa tenzi za kuomboleza, kisha muili wake ukazungushwa katika malalo takatifu, mbele ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na idadi kubwa ya wajumbe wa kamati kuu na wafanyakazi wa malalo hiyo tukufu.

Halafu muili wake ukabebwa hadi kwenye malalo ya babu yake Imamu Hussein (a.s) kwa kupitia katika uwanja wa katikati ya haram mbili, nakufanyiwa kama alivyo fanyiwa katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s). Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulikua umesha tangaza msiba wa Sayyid Jaasim Towirajawi.

Marehemu Towirajawi anaitwa Sayyid Jaasim bun Sayyid Abdu bun Sayyid Abbasi Al-Ardawi, anatokana na familia ya masayyid ambao nasaba yao inaenda hadi kwa Imamu Hussein (a.s), alizaliwa katika mji wa Najafu Ashrafu mwaka 1947, alikuwa na elimu ya sekula na ya hauza, alisoma elimu ya tablighi, usulu na uhadhiri mwishoni mwa miaka ya hamsini kwa mhadhiri mkubwa Shekh Muhammad Ali Ya’qubi na kwa mhadhiri Sayyid Hussein Jawadi, kisha aliishi na wahadhiri wa kipindi cha harakati za kifikra katika mji wa Najafu na Furaat ya kati, kwa mfano Dokta Shekh Ahmadi Waailiy, na Shahidi Sayyid Jawadi Shibri, na Shahidi Shekh Abduzaharaa Kaabiy, na Sayyid Murtadha Qazwini.

Katika mihadhara yake alikua anatumia njia ya ufafanuzi wa kina kwa lugha rahisi kueleweka na kila mtu katika jamii, alitumia zaidi maneno ya upole kutoka kwa Maimamu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), hadi akajulikana kwa sifa ya muimbaji wa tenzi za Twafu na mtumishi wa majaalisi za bibi yake Zaharaa (a.s).

Kwa kifo cha Sayyid Towirajawi uwanja wa wahadhiri wa Najafu na Karbala pamoja na Iraq kwa ujumla umepoteza hazina kubwa iliyo chomoza katika harakati za uhadhiri kwenye miaka ya stini na sabini karne iliyopita, aliyekuwa mashuhuri kwa msimamo wake wa kulinda turathi za uombolezaji kwa kufuata mwenendo wa upole katika kueleza misiba na mitihani waliyopata Maimamu wa Ahlulbait (a.s), muimbaji wa tenzi za Twafu ajulikanae kama mhadhiri wa Zaharaa na watoto wake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: