kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya: Huduma ya matangazo mubashara imenufaisha vyombo vingi vya habari wakati wa ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
kitengo cha habari katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kuwa makumi ya chanel za luninga kutoka ndani na nje ya Iraq, zimenufaika na masafa ya kurusha matangazo bure iliyo tengenezwa na kitengo hicho.

Makamo rais wa kitengo hicho Ustadh Ahmadi Swadiq akasema: “Kituo cha uzalishaji wa vipindi na matangazo mubashara Alkafeel, kilikua na mchango mkubwa kwa kuandaa mfumo wa kurusha matukio ya ziara ya Arubaini, kupitia masafa maalum ya bure, miongoni mwa sifa za masafa hiyo ni:

  • - Kurusha mubashara matukio ya ziara ya Arubaini, chini ya ratiba ya kurusha matukio hayo kuanzia kituo cha mbali hadi Karbala.
  • - Kurusha matangazo ya kuomboleza kutoka ndani ya malalo mbili takatifu na harakati za mawakibu za kuomboleza.
  • - Kurusha vipande vya kuomboleza vilivyo andaliwa kabla na wakati wa ziara.
  • - Kuandaa na kurusha matukio ya huduma zinazo tolewa na Atamatu Abbasiyya pamoja na malengo ya ziara hii.
  • - Kutengeneza vipande vifupi vifuti vya filamu, vinavyo onyesha matembezi hayo pamoja na malengo ya ziara hiyo”.

Akasisitiza kuwa: “Huduma hiyo imenufaisha makumi ya vyombo vya habari ndani na nje ya Iraq, idadi ya chanel zilizo nufaika mwaka huu imezidi idadi ya chanel zilizo nufaika mwaka jana, hii inatokana na uzowefu walionao watumishi wa sekta hiyo, pamoja na vifaa vinavyo milikiwa na kituo, vyenye uwezo mkubwa unaokidhi viwango vinavyo takiwa na vyombo vya kimataifa, na kuvifanya vipende kurusha matangazo hayo ya ziara inayo hudhuriwa na mamilioni ya watu”.

Akabainisha kuwa: “Kamati ya habari katika Atabatu Abbasiyya tukufu imesaidia sana vyombo vingine vya habari kwa kutumia gari zake na wataalamu wake kufusha matangazo ya mubashara, wamepata picha bila tatizo lolote, matangazo hayo yalikuwa yanapatikana pia kupitia youtube na mitandao ya mawasiliano ya kijamii kwa ubora mkubwa uliowezesha vyombo vya habari kunufaika na vipindi hivyo”.

Akamaliza kwa kusema: “Kituo cha mawasiliano kilicho chini ya kitengo chetu kilikuwa na nafasi muhimu, katika kupokea waandishi wa habari wa vyombo tofauti vya kitaifa na kimataifa na kuwarahisishia utendaji wao”.

Kumbuka kuwa kituo cha uzalishaji na matangazo mubashara Alkafeel kinamiliki masafa yake maalum, kinarusha matangazo yake bure kupitia masafa hiyo katika kila msimu wa ziara.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: