Kuanza utengenezaji wa dirisha la bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Kitengo cha kutengeneza madirisha ya makaburi na milango chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimeanza kutengeneza dirisha jipya la kaburi la bibi Zainabu (a.s), baada ya kumaliza kutengeneza taji na paa pamoja na kuviweka juu ya kaburi hilo.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo hicho Sayyid Naadhim Ghurabi amesema kuwa: “Hakika kuanza kazi hii kumetokana na ubora wa kazi za awali, mafundi wa kitengo hiki watatumia ujuzi wao wote kufanikisha mradi huo, unaotarajiwa kuingia katika orodha ya mafanikio ya kiwanda hiki, tena yanayo kotana na kasi zinazo fanywa na raia wa Iraq na watumishi wa Ahlulbait (a.s)”.

Akaongeza kuwa: “Kazi ya kwanza katika mradi huu ilikua ni kufanya usanifu wa dirisha hilo, linalo tarajiwa kuwa zuri zaidi ya dirisha lililopo sasa, mafundi kapenta nao wameanza kutengeneza mbao za dirisha hilo, kazi hiyo ndio msingi wa kuendelea katika hatua zingine za kutengeneza sehemu za madini na mbao, tumechagua aina bora zaidi ya mbao za (Burumi), zinatengenezwa kwa kiwango kinacho endana na uzito utakao wekwa juu yake”.

Akafafanua kuwa: “Jengo la mbao lina nguzo nne kubwa na kumi ndogo zinazo tenganisha madirisha, pamoja na ngazi nne za mbao za kulala zinazo shika nguzo, zinazo unganishi baina yake na madini kwa ujazo wa (ml5) ili kuifanya kuwa imara zaidi na kudumu muda mrefu, pamoja na mbao zingine nne za kulala, ambazo zinabeba ngozo nne kubwa”.

Akasisitiza kuwa: “Kazi inaendelea vizuri kama ilivyo pangwa, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu itakamilika hatua moja baada ya nyingine”.

Kumbuka kuwa mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wanaofanya kazi katika kiwanda cha kutengeneza madirisha ya makaburi na mazaru matukufu, wanauzowefu mkubwa wa kufanya miradi ya aina hii, wamefanikiwa kuonyesha ufanisi wao kwa vitendo, pale walipo tengeneza dirisha la kaburi takatifu la Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na madirisha ya Swafi-Swafa, halafu wakatengeneza dirisha la Qassim (a.s) na milango ya malalo ya Sayyid Muhammad –Sabú-Dujail- na dirisha la malalo ya Shekh Mufiid na Shekh Tusi, bila kusahau sehemu ya juu ya dirisha la maimamu wawili Jawadaini (a.s) pamoja na kazi zingine nyingi, ikiwemo sehemu ya mbele ya dirisha la Maqaam ya Imamu Mahadi (a.f), na paa pamoja na taji la juu ya dirisha la malalo ya bibi Zainabu (a.s), sambamba na kazi zinazo endelea sasa hivi kama vile dirisha la Maqaam Kafu na dirisha upande wa wanawake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: