Kwa picha: Mazuwaru wameanza kumiminika katika mji wa Najafu Ashrafu wakitembea kwa miguu

Maoni katika picha
Njia zinazo elekea katika mji wa Najafu zinashuhudia idadi kubwa ya mazuwaru wanaokwenda kuzuru haram ya kiongozi wa waumini (a.s), kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha mpenzi wake na ndugu yake mtoto wa Ammi yake Mtume wa rehma Muhammad (s.a.w.w), ambaye tarehe ya kifo chake inasadifiana na siku ya Ijumaa ijayo (mwezi 28 Safar 1442h).

Mawakibu za kutoa huduma zimeweka mahema kwenye barabara zote zinazo elekea Najafu kwa ajili ya kutoa huduma mbalimbali kwa mazuwaru hao.

Tambua kuwa miongoni mwa suna bora zinazo tajwa na riwaya zilizo pokelewa kutoka kwa Ahlulbait (a.s), ni ziara ya kiongozi wa waumini (a.s) katika kumbukumbu hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: