Kitengo cha Dini: Tuligawa maelfu ya machapisho kwa mazuwaru wakati wa ziara ya Arubaini

Maoni katika picha
Kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kuwa kiligawa maelfu ya machapisho mbalimbali kwa mazuwaru, kupitia vituo vya tablighi ilivyo fungua wakati wa ziara ya Arubaini.

Kiondozi wa idara ya tablighi katika kitengo hicho Sayyid Muhammad Abdullahi Mussawi amesema kuwa: Vituo vya tablighi havikuishia kujibu maswali ya kidini na kiitikadi na kuongoza mazuwaru peke yake, bali kulikua na harakati zingine, pamoja na kwamba harakati ya kwanza ndio muhimu zaidi, sambamba na harakati hizo tuligawa machapisho yenye mafundisho ya kidini na kiitikadi.

Akaongeza kuwa: Miongoni mwa machapisho tuliyo gawa yapo yanayo husiana na ibada ya ziara na malengo yake pamoja na njia za kunufaika nayo, na mengine yanaeleza hukumu za maadhimisho na mambo yanayo husiana na hijabu sanjari na maadhimisho ya Husseiniyya.

Kumbuka kuwa kitengo cha Dini kiliweka vituo kwenye maeneo mengi ya barabara zinazo elekea Karbala, vituo hivyo vilikua na jukumu la kujibu maswali ya mazuwaru kidini na kijamii, na kutoa maelekezo ya ki-Fiqhi au Aqida au Akhlaqi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: