Idara ya mawasiliano na teknolojia inabainisha mitambo iliyotumia kuhesabu mazuwaru

Maoni katika picha
Idara ya mawasiliano na teknolojia chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imetaja mitambo iliyotumia kuhesabu watu waliokuja kufanya ziara ya Arubaini mwaka huu, ambao walikua zaidi ya milioni (14).

Kiongozi wa idara hiyo Mhandisi Farasi Abbasi Hamza amesema kuwa: “Kuna wanaohoji kuhusu utendaji wa mitambo ya kuhesabu watu kielektronik iliyotumika kuhesabu mazuwaru, kila unapokaribia msimu wa ziara kubwa huwa tunafunga kamera za teknolojia ya kisasa zenye uwezo mkubwa ndani ya mji mtukufu wa Karbala, zenye jukumu la kuhesabu mazuwaru chini ya jopo la wataalamu wa kazi hiyo, wenye uwezo na uzowefu mkubwa wa kutumia kamera hizo na kupata majibu sahihi”.

Akabainisha kuwa: “Kuna aina nyingi za kamera na kila moja inajukumu lake kama tutakavyo bainisha.

Aina ya kwanza: Kuhesabu watu (people counting) hufungwa katika njia zinazo tumiwa na mazuwaru kutembea kwa miguu, zinauwezo mkubwa wa kuhesabu watu na kuhifadhi kwenye ukurasa maelezo, sambamba na kuhesabu watu kwa kuwaangalia kwa muda wa dakika tano katika kila saa, kisha tunaangalia uwiyano wa idadi ya kuhesabu kwa macho na kwa kamera, kuna wakati hutokea tofauti katika usomaji wa kamera, mara nyingi wakati wa usiku kwenye (correction factor) kutokana na udhaifu wa mwanga pamoja na asilimia kubwa ya mazuwaru kuvaa nguo nyeusi, huwa tunafanya marekebisho na kuweka idadi inayodhaniwa iko sawa.

Aina ya pili: Kuhesabu magari (vehicle counting), nazo hufungwa ndani ya mji mtukufu wa Karbala, na kuelekezwa kwenye barabara zinazo tumiwa na gari, kamera zinazo tumika kuhesabu gari zinauwezo mkubwa, utambuzi wa watu waliomo ndani ya gari hufanywa kutokana na ukubwa wa gari, na huwekwa makadirio ya chini kulingana na gari husika, mara nyingi gari ndogo hukadiriwa kuwa na watu (4) na basi kubwa za ghorofa hukadiriwa watu (80), pia huwa tunafatilia katika idara inayo husika na ukaguzi wa gari zinazo ingia kupitia ukurasa maelezo, kwa mfano zinapo ingia gari elfu moja na ikawa asilimia %10 ni gari ndogo na asilimia %30 gari za (viti 11), asilimia %50 za (viti 21), asilimia %10 basi za (viti 40), kiwango cha chini kitakua ni (18200), idadi hiyo inakaribia uhalisia wa idadi ya watu wanao weza kubebwa na gari hizo”.

Katika kumaliza maelezo yake akasema: “Kamera huwa sio za kukaa mahala pamoja, kwa sababu wakati mwingine baadhi za barabara hufungwa na watu kuhamishiwa katika barabara za watembea kwa miguu, hapo hutumika kamera zinazo endana na hali hiyo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: