Mawakibu za kuomboleza za Karbala zinakumbuka kifo cha Mtume mbele ya kaburi la Imamu Ali (a.s)

Maoni katika picha
Kama kawaida yao ifikapo jioni ya siku kama ya leo mwezi ishirini na nane Safar katika kila mwaka, maukibu za watu wa Karbala, huomboleza msiba mkubwa wa kufiwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w), na kutoa rambirambi kwa mtoto wa Ammi yake na ndugu yake kiongozi wa waumini Ali (a.s) mbele ya kaburi lake takatifu katika mji wa Najafu, kwa kushirikiana na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.

Rais wa kitengo cha mawakibu na vikundi vya Husseiniyya bwana Riyadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Maukibu za kuomboleza za watu wa Karbala ni miongoni mwa mawakibu ambazo Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimezowea kuzisaidia katika shughuli za uombolezaji, hususan zinazo fanywa nje ya mkoa kwenye matukio tofauti, likiwemo tukio la kuomboleza kifo cha Mtume Muhammad (s.a.w.w)”.

Akaongeza kuwa: “Waombolezaji wamefanya majlisi ndani ya haram ya kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), wameimba kaswida na tenzi zilizo onyesha ukubwa wa msiba huu, sambamba na kuongea maneno ya kuomboleza na huzuni katika kuwapa pole Ahlulbait (a.s) kutokana na msiba huu”.

Akabainisha kuwa: “Msafara wa maukibu ulianza matembezi kutokea sehemu yake maalum inapo anzia kila mwaka, nayo ni katika Husseiniyya ya watu wa Karbala kwenye barabara ya Tusi, baada ya kusimama na kujipanga vizuri walianza kutembea huku wakiimba kaswida zilizo amsha huzuni na kuonyesha ukubwa wa msiba huu katika nafsi za waumini”.

Akamaliza kwa kusema: “Ataba mbili tukufu zimeandaa gari (45) zenye ukubwa tofauti kwa ajili ya kubeba waombolezaji kutoka Karbala hadi Najafu, halafu kutoka Najafu hadi kwenye mji wa Qassim (a.s) na kuomboleza huko kama walivyo fanya katika mji wa Najafu, hii ndio desturi iliyo zoweleka katika kuomboleza msiba huu, sambamba na kuwapa chakula”.

Kumbuka kuwa maukibu hii ya kuomboleza ni utamaduni wa kila mwaka, watu wa Karbala huadhimisha matukio mbalimbali yaliyo wakumba Ahlulbait (a.s), kupitia maukibu zinazo undwa na vikundi tofauti vya Husseiniyya katika mji mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: