Waziri wa afya: Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamethibitisha kuwa wao ni makamanda wakati wote

Maoni katika picha
Waziri wa afya wa Iraq Dokta Hassan Tamimi amesema kuwa, hakika watumishi wa Atabatu Abbasiyya ni makamanda katika kila wakati, wanastahiki pongezi katika mambo mengi, kama walivyo simama imara kupigana na magaidi wa Daesh, wakasaidia kuwashinda na kukomboa miji waliyokua wameiteka hapa Iraq, leo watumishi hao wamesimama imara kusaidia taasisi za wizara ya afya kupambana dhidi ya janga la Korona, miongoni mwa kazi kubwa ambayo wamefanya katika vita hii ni ujenzi wa vituo saba vya kutibu watu walio ambukizwa virusi hivyo, kwa hakika vimesaidia sana kupunguza msongamano uliokuwepo katika hospitali zetu.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa kituo cha Alhayaat katika mji mkuu wa Bagdad, uliofanywa asubuhi ya Jumamosi (17 Oktoba 2020m) sawa na mwezi (29 Safar 1442m), katika eneo la Raswafa, kilicho jengwa na kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (5000) kina vyumba vya wagonjwa (118) na vyumba (19) vya madaktari na wauguzi pamoja na ofisi, ujenzi huo umekamilika ndani ya siku (55).

Akaongeza kuwa: “Jengo hili linamambo mengi mazuri, ikiwa ni pamoja na mapambo yake ya kiujenzi, ubora wa vifaa vilivyo tumika, sambamba na kukamilika ujenzi ndani ya muda mfupi. Mafundi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wamejenga jengo kama hili katika mkoa wa Karbala, Najafu, Baabil, Muthanna na Bagdad, bado kuna miradi mingine inaendelea, hakika ni fahari na heshima kwa wairaq wote kutokana na utendaji wa miradi tofauti unaofanywa na watumishi hao”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: