Kwa ukubwa wa vitanda 120: Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua jengo la Alhayaat la tano kwa ajili ya kutibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona na kulikabidhi kwa wizara ya afya

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Jumamosi mwezi (29 Safar 1442h) sawa na tarehe (17 Oktoba 2020m) imefanya ufunguzi wa jengo la Alhayaat la tano, ambalo ni kituo cha kutibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona katika mkoa wa Bagdad, lililojengwa katika eneo la hospitali ya ibun Qafu chini ya idara ya afya ya Raswafa, baada ya kukamilisha ujenzi wake ndani ya muda mfupi na kwa ubora mkubwa unao endana na malengo ya ujenzi huo, uliofanywa na mafundi wa kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ujenzi umefanywa kwenye kiwanja chenye ukubwa wa mita (5000), na ujenzi umekamilika ndani ya siku (55), jengo linajumla ya vitanda (120), vyumba bya wagonjwa (118) na vyumba (19) vya madaktari na wauguzi.

Ufunguzi huo na makabidhiano umehudhuriwa na waziri wa afya wa Iraq Dokta Hassan Tamimi na ugeni uliowakilisha Atabatu Abbasiyya tukufu ulio husisha wajumbe wa kamati kuu na marais wa vitengo pamoja na mkuu wa idara ya afya ya Raswafa na wawakilishi wawili kutoka serikali ya eneo hilo bila kumsahau mkuu wa hospitali ya ibun Qafu.

Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya ulifuatana na waziri pamoja na watu walio ongozana nae katika kutembelea sehemu za jengo hilo, na wakatoa maelezo kwa ufupi kuhusu ujenzi huo na namna walivyo fanikiwa kukamilisha ndani ya muda mfupi wa siku (55) tu pamoja na changamoto zote walizo kuwa nazo.

Baada ya kumaliza kutembelea sehemu mbalimbali za jengo hilo walifanya kikao na waandishi wa habari wa vyombo tofauti vya redio, magazeti na luninga, waziri alianza kwa kusifu Atabatu Abbasiyya tukufu, na kueleza mchango wake katika vita dhidi ya janga la Korona, na moja ya vielelezo vya mchango wao ni ujenzi wa kituo hiki cha Alhayaat cha tano.

Naye mjumbe wa kamati kuu ya Atabatu Abbasiyya Dokta Abbasi Rashidi Mussawi akasema kuwa, Hakika ujenzi wa kituo cha Alhayaat cha tano katika mkoa wa Bagdad kwa ajili ya kutibu watu walio ambukizwa virusi vya Korona ni zawadi kwa raia wa Iraq, na kuonyesha kusimama pamoja nao katika mazingira haya magumu, aidha ni mrejesho mzuri kwao kutokana na Imani yao kwa watumishi wetu.

Rais wa kitengo cha usimamizi wa majengo ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya, akataja sifa muhimu za jengo hilo, ambalo limejengwa na watumishi wa kitengo chake kwa muda mfupi na kwa ubora wa hali ya juu.

Naye mkuu wa idara ya afya ya Raswafa Dokta Abdulghina Saaidiy akasema kuwa, jengo hili ni fahari kubwa kwa wizara ya afya na raia wote wa Iraq, kutokana na huduma zitakazo tolewa ndani ya jengo hili katika kipindi hiki cha janga la Korona hata baada ya kuisha janga hili.

Kumbuka kuwa jengo la Alhayaat la tano ni miongoni mwa majengo makubwa yaliyo jengwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, nalo ni moja ya majengo saba yaliyo jengwa na mafundi wa Atabatu Abbasiyya kwenye mikoa tofauti: Baabil, Muthanna, mji wa Imamu Hussein (a.s) wa kitabibu majengo mawili, na katika hospitali ya Hindiyya mkoani Karbala, na jengo lililojengwa kwa ufadhili wa hospitali ya kiongozi wa waumini (a.s) katika mkoa wa Najafu, ujenzi huo ni sehemu ya kufanyia kazi maelekezo ya Marjaa Dini mkuu na muongozo wa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, wa kusaidia watumishi wa afya katika kupambana na janga la Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: