Ofisi ya Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Sistani imetangaza kuwa, haijathibiti kuonekana mwezi kwa macho hapa Iraq na nchi jirani baada ya kuzama jua siku ya Jumamosi ya mwezi (29 Safar), hivyo kesho siku ya Jumapili ni siku ya mwisho katika mwezi huu na Jumatatu itakua siku ya kwanza ya mwezi wa Rabiul-Awwal 1422h, Mwenyezi Mungu aufanye kuwa mwezi wa kheri na baraka kwa waislamu wote.