Imekua desturi kuhuisha msiba wa Husseiniyya katika siku kumi za kwanza ndani ya mwezi wa Muharam, kuwa ni siku maalum za mawakibu na vikundi vya Husseiniyya vya watu wa Karbala, na ziara ya Arubaini huachiwa mawakibu za kutoa huduma na kuomboleza zinazo kuja Karbala kutoka mikoa mingine au nje ya nchi.
Jambo hilo halizuwii ushiriki wa mawakibu za Karbala kutoa huduma kwa mazuwaru, mwaka huu jumla ya maukibu (1489) zimetoa huduma katika barabara zinazo elekea kwenye malalo mbili takatifu, hizo ndio zilizo sajiliwa na kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya, na zikasimama bega kwa bega na mawakibu za mikoa mingine, aidha kuna nyumba za makazi ya watu na Husseiniyya nyingi zilizo fungua milango na kuhudumia mazuwaru.
Bwana Riyadh Ni’mah Salmaan ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika watu wa Karbala na mawakibu zao wanamchango mkubwa katika kuhudumia mazuwaru wa ziara hii na zinginezo, kutokana na mazingira ya ziara hii, wameshiriki kwa namna kubwa kutoa huduma mbalimbali, wazee, vijana, wanawake kwa wanaume wamehudumia mazuwaru wa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), wamejitolea kila walicho nacho katika kuwahudumia mazuwaru kipindi chote cha ziara, baada ya kuondoka mawakibu za kutoa huduma wao wameendelea kuwahudumia mazuwaru waliokuja siku za mwisho”.