Kazi kubwa imefanywa na watumishi wa tawi la wanawake katika mgahawa wa nje wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Maoni katika picha
Watumishi wa tawi la wanawake wanaofanya kazi katika mgahawa wa nje wa Atabatu Abbasiyya chini ya kituo cha Swidiiqah Twahira (a.s) wamefanya kazi kubwa wakati wa ziara ya Arubaini na baada yake, kwa kutoa huduma bora kwa wanawake waliofika kwenye mgahawa huo, sambamba na kuzingatia masharti ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Tumeongea na kiongozi wa kituo cha wanawake bibi Zainabu Ardawi kuhusu huduma walizo toa, amesema kuwa: “Mwaka huu tumetoa huduma tofauti na miaka mingine, kwa sababu ya janga la maambukizi ya virusi vya Korona, tulianza kutoa huduma mwezi saba Safar hadi mwisho wa ziara na baada yake”.

Akaongeza kuwa: “Kabla ya kila kitu, tumezingatia kwa kiwango kikubwa masharti yote ya kujikinga na maambukizi ili kuwalinda mazuwaru, ikiwa ni pamoja na kupuliza dawa, kuvaa barakoa na sokri za mikononi, pamoja na kupuliza matandiko yanayo tumiwa na mazuwaru mara mbili kwa siku, tunafanya kila kitu kilicho elekezwa na kamati ya afya ikiwa ni pamoja na kupima hali ya joto za mazuwaru”.

Akaendelea kusema: “Tulipunguza idadi ya watu wanaolala na tukajenga hema jirani yetu ili tuweze kupokea idadi kubwa zaidi ya mazuwaru”.

Akafafanua kuwa: “Mazuwaru walikuwa wanaingia kwa utaratibu maalum kupitia mistari, na kila aliyekuwa anaingia alipuliziwa dawa, na kukaribishwa sehemu ya kupumzika, watumishi wetu wanauzowefu mkuwa wa kuhudumia mazuwaru”.

Tambua kuwa wahudumu wa mgahawa huo wanatoka kituo cha Swidiiqah Twahirah pamoja na wakina mama kutoka idara ya Quráni ambayo iko chini ya shule za Alkafeel, na baadhi ya wanawake wanaojitolea katika mkoa wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: