Kuondoa vazi la huzuni na mapambo meusi katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Baada ya kumaliza msimu wa huzuni za watu wa familia ya Mtume Muhammad (a.s) na kutangazwa kuandama mwezi wa Rabiul-Awwal, tumeondoa vazi la huzuni na mapambo meusi yaliyokuwa yamewekwa ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na maeneo yanayo izunguka, ambayo yamekaa kwa kipindi cha miezi miwili Muharam na Safar, kuondolewa kwa mapambo hayo ni tangazo la kuisha msimu wa huzuni kwa watu wa familia ya Mtume Muhammad (a.s) na kuupokea mwezi wa Rabiul-Awwal.

Kazi hiyo imefanywa kwa awamu, walianza kuondoa katika maeneo yanayo zunguka Atabatu Abbasiyya, halafu wakaja katika sehemu za ndani ya jengo tukufu la haram kwa kuanzia kwenye dirisha takatifu, wameondoa mapambo yote meusi yanayo maanisha alama ya msiba na huzuni yaliyokua yamewekwa ndani ya haram tukufu, na wakamalizia kwa kubadilisha bendera takatifu ya Kubba, wametoa bendera nyeusi iliyokua imeandikwa (Ewe mnyweshaji wenye kiu Karbala), na kuweka bendera nyekundu iliyo andikwa (Ewe mwezi wa bani Hashim) yenye ukubwa sawa na nyeusi, pamoja na kuzima taa nyekundu na kuwasha za kijani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: