Jopo la madaktari wa hospitali ya rufaa Alkafeel limefanikiwa kufanya upasuaji wa kibiongo na kuondoa kupinda kwa mgongo wa mgonjwa mwenye umri wa miaka thelathini.
Daktari bingwa wa upasuaji uti wa mgongo katika hospitali hiyo Dokta Waaili Qassim amesema kuwa: “Jopo la madaktari wetu limefanikiwa kuondoa kibiongo cha mgonjwa mwenye umri wa miaka thelathini”.
Akabainisha kuwa: “Upasuaji huo umefanywa chini ya uangalizi wa mtambo maalum”.
Akaongeza kusema: “Upasuaji umechukua saa nane chini ya madaktari bingwa na wenye uzowefu mkubwa, pamoja na vifaa tiba vya kisasa vilivyo tushajihisha kufanya upasuaji huo”.
Akasema: “Mgonjwa alikuwa ameshawahi kufanyiwa upasuaji sehemu nyingine bila mafanikio”.
Akasisitiza kuwa: “Upasuaji wetu umefanikiwa kuondoa kibiongo cha mgonjwa na ameweza kusimama akiwa amenyooka vizuri na mwenye afya njema”.
Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inajitahidi kutoa huduma bora wakati wote kupitia vifaa tiba vya kisasa ilivyo navyo na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi, jambo hili limeiwezesha kutoa ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa.
Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa wa magonjwa tofauti kila wakati, sambamba na kupokea wagonjwa ambao wapo katika hali mbalimbali za maradhi yao.